Tanganyika tuliuza jina, Zanzibar wakauza nchi

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,864
Mwl Nyerere alikuwa mjanja sana. Yeye hakujali kuuza jina la nchi ya Tanganyika maana kuna nchi kama Rhodesia ilibadili jina na kuwa Zimbabwe na Zaire ikawa Congo DRC. Hivo yeye alimdanganya Karume akauza nchi!

Zanzibar ni nchi ya kwanza kupokea dini ya kikristo kabla ya nchi zote za Afrika Mashariki na nchi ya kwanza kupokea dini ya kiislam kabla ya nchi zote Afrika ukiondoa zile ambazo raia wake ni waarabu. Ni nchi ya kihistoria na nisingeshangaa kama ingekuwa Dubai ya Afrika kama si kuiuza kwa Tanganyika.

Leo Tanganyika kwa kushirikiana na wazanzibari wachache hawaiachi ipumue wanahakikisha anayeongoza Zanzibar ni yule anayekubalika Dar es Salaam. Aliyefunga ndoa na Ccm, hivi Ccm ni chama cha wazanzibari (itakuwa mada ya siku nyingine).
 
Dah, jamani haya mambo yatampelemka mtu TCRA, me simo, Shauri yenu!
 
Tanganyika ni jina lilitungwa na wakoloni. Tanga za kupokea upepo na kuendesha mashua za baharini. Nyika ikiwa bara. Wakaunganisha wakapata tanganyika. Hakukuwepo na tanganyika kulikuwa na wazaramo wachaga wagosi wahehe sukuma pare wagogo etc. Tanganyika bora Nyerere alilifukia mbali na sitaki lirudi. Japo nasikia kulikuwa na Azania sasa hapo ndio nachanganyikiwa, Azania sijui ilikuwa ni kabla ya wazungu na ilikuwa inajimuisha maeneo gani, mtu anaejua aelezee.
Tanzania itabaki milele, to hell with tanganyika, hata masherehe ya uhuru tuachane nayo.
 
Kama ni hivo Tanzania ni nini?
 
Dah, jamani haya mambo yatampelemka mtu TCRA, me simo, Shauri yenu!
Shida ya watanzania ni woga na kwa mjibu wa Lema woga ni dhambi kubwa kuliko zote. Watanzania tumejua mambo mangapi ambayo kama si Lissu kuondoa woga tusingeyajua kuhusu Zanzibar
 
Huu ni ukweli mtupu, ngoja niwaombee wazanzibari ili waamke na kuikomboa nchi yao, eeeeh Mungu wangu wasaidie wazanzibari waweze kujitambua haraka ili waikomboe nchi yao ambayo sisi watanganyika tunaitawala kwa mabavu kupitia watu wachache tuliowaweka huko zanzibar eeeeh Mungu wangu naomba uwasaidie, amen
 
Shida ya watanzania ni woga na kwa mjibu wa Lema woga ni dhambi kubwa kuliko zote. Watanzania tumejua mambo mangapi ambayo kama si Lissu kuondoa woga tusingeyajua kuhusu Zanzibar
Kunguru muoga huishi miaka mingi.
 
Huu ndiyo ukweli usiopingika, Karume angezijua hila za mwalimu akamwepuka miaka ile ya 1964 leo hii katika Afrika Zanzibar isingekuwa inakamatika kimaendeleo.

Lakini tangu alipoinunua mpaka leo wazanzibar wanaishi kama manamba wa enzi za mkonge Tanga.

Ukimtazama Rais wa Zanzibar akihutubia kheri ya Makonda anahubiri kwa kujiamini.

Ila kidogo huko mbeleni bi Fatma Karume atayafuta makosa yaliyotendwa na babu yake tumpe muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…