TANESCO yatoa siku nne kwa wadaiwa sugu kulipa madeni

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA ( TANESCO) TAARIFA KWA UMMA - WADAIWA SUGU

Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

Mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

JANUARI 11, 2018
 
Back
Top Bottom