TANESCO yatangaza kuzima umeme katika Wilaya mbalimbali za Geita siku ya Jumamosi

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
861
2,330
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuzimwa kwa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Shinyanga hadi Bulyanhulu, pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Bulyanhulu, Geita, na Nyakanazi.

Hatua hii inatokana na matengenezo ya kuunganisha transfoma mpya katika kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu.

Huduma ya umeme itakatika kwa muda wa saa nne siku ya Jumamosi, tarehe 30 Novemba 2024, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.

Maeneo yatakayokumbwa na ukosefu wa umeme ni pamoja na Mkoa wa Geita na wilaya za Kibondo, Kasulu, Kakonko, Ngara, na Biharamulo, pamoja na mgodi wa Bulyanhulu Goldmine.

Soma pia: TANESCO Geita kuna shida gani? Mbona umeme unakatika sana?


20241128_162740.jpg
 
Dah!Sasa wasukuma wataendaje kucheza ngoma za mbina?Wasukuma wanaonewa sana.Wanunue vibatari kabla giza halijaleta noma!
 
Back
Top Bottom