ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 61,760
- 72,193
Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza mazungumzo na Kampuni ya TAQWA-DALBIT kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa upatikanaji wa nishati ya umeme migodini na maeneo yenye wachimbaji wadogo ili kuchochea shughuli za uchimbaji madini nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika Februar 14, 2024 Jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde na Naibu Waziri Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa pamoja na Menejimenti ya Vongozi wa Kampuni ya TAQA-DALBIT ikiongozwa na Meneja Mkuu Ndugu Amr Aboushad na Mkurgenzi wa maendeleo ya Biashara Ndugu Raphael Banzi.
Akiwasilisha maelezo ya awall, Nougu Amr Aboushad alisema kwamba kampuni yao ipo tayari kuja na mpango wa uzalishaji wa umeme kupitia gesi kwa kufunga mtambo katika migodi na maeneo ya wachimbaji ambayo itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa zaidi ya nusu ya gharama inayotumika hivi sasa kupitia matumizi ya mafuta ya dizeli na petroli na awamu ya pili itahusisha uzalishaji wa umeme kupitia mfumo wa umeme jua ambapo Kampuni itafunga mtambo mkubwa kwa gharama yao na kuwaunganisha wachimbaji wadogo kwa malipo ya mwezi ya matumizi ya nishati hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameishukuru Kampuni ya TAQA-DALBIT kwa utayari wa kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme migodini na kuagiza uongozi wa Wizara kuitisha mkutano wa haraka na wadau wote wakiwemo wachimbaji wadogo na wakubwa ili kupata fursa ya kujadiliana namna bora ya utekelezaji wa mpango huu.
Utekelezaji wa mango hu utasaidia sana kuchochea shughuli za chimbaji chini Tanzania na hivyo kuongeza uzalishaji wa madini.
===
Serikali Kupitia Wizara ya Madini imeamua kuachana na Tanesco na kutafuta mzalishaji na msambazaji wa umeme migodini.
TAQWA-DALBIT Wamesainiana MoU na Wizara ya Madini kuanza kazi hiyo.
Maoni Yangu.
Binafsi sikubaliani na hii Kwa sababu huenda ikawa ni Mpango wa Wanasiasa kujinufaisha na kudidikiza Tanesco Kwa makusudi.
Kwa nini makubaliano yafanyike Sasa wakati bwawa linaenda kukamilika na umeme wa bwerere utakuwepo?
Pili migodi na viwanda ndio sehemu ya uhakika Kwa Tanesco kupata pesa kuliko Kwa individuals consumers ambao Kwa mujibu wa Tanesco wanauziwa umeme Kwa bei ya ruzuku,Je hii sio hujuma ya makusudi?
Tatu, Kwa nini hao TAQWA-DALBIT wasipewe tender ya kujenga miundombinu huko kwenye migodi eg distribution lines Ili kurahisishia Tanesco kuunga umeme?
Kuna harufu ya Ufisadi na Wanasiasa kujinufaisha.Bunge kataeni hili Dili haramu.