TANESCO yakemea upotoshaji kuhusisha mafuriko Pwani na JNHPP

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
9,053
4,858
TANESCO yakemea upotoshaji kuhusisha mafuriko Pwani na JNHPP

DODOMA: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limefafanua kuwa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari za mafuriko katika maeneo ya Wilaya za Rufiji na Kibiti, tofauti na kinyume chake inavyoripotiwa kuwa mradi huo umechangia kutokea kwa mafuriko hayo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa TANESCO, Makao Makuu Dodoma leo imeeleza kuwa kitakwimu inaonesha kuwa maeneo ya Rufiji na Kibiti mkoani Pwani yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kwa miaka mingi ya nyuma kwa kiwango kikubwa kuliko hali ilivyo hivi sasa.

“Kama mradi wa JNHPP usingejengwa basi maji haya yangefika moja kwa moja kwenye maeneo ya Rufiji na Kibiti na hivyo kusababisha athari kubwa zaidi,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa athari za mafuriko zinazoonekana sasa zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha tangu mwaka jana hivyo kupelekea mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.

“TANESCO inakanusha taarifa zozote za upotoshaji zinazohusisha bwawa la Julisu Nyerere na mafuriko ya Kibiti na Rufiji na linakemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasio na nia njema kubeza juhuhudi za serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwa ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere,” imekemea taarifa hiyo
 
TANESCO yasema mradi JNHPP umesaidia kupunguza athari mafuriko Rufiji,Kibiti
By Frank Monyo , Nipashe
Published at 06:43 PM Apr 11 2024

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu athari za mafuriko yanayoendelea katika maeneo ya wilaya za Rufiji na Kibiti ambayo yanahusishwa na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Kupitia taarifa yake kwa Umma, TANESCO imesema kuwa "Tunapenda kuujulisha umma kwamba uwepo wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere umesaidia kwa sehemu kubwa kupunguza athari ya mafuriko katika wilaya za Rufiji na Kibiti ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla mradi haujajengwa.

IMG-20240411-WA0015.jpg 177.89 KB
 
Ukweli ni kuwa Tanesco wanahusika kwa 100% katika mafuriko haya yaliyoangamiza makumi ya vijiji huko Rufiji.

Kwa nini hawakufungulia maji mapema ili maji yanayokuja bwawani yahifadhiwe, badala yake wakangojea bwawa lijae ndipo wafungulie na kusababisha maji yaliyoko bwawani na maji ya mvua zinazoendelea kuvamia vijiji.

Utabiri wa hali ya hewa ulikwisha kuonyesha mvua nyingi zaidi zinakuja lakini wakakaza shingo na kufurahia kujaa maji bila kujali maafa yanayokuja.

Kwa hili lililotokea lawama zote kwa Tanesco!
 
HATUDANGANYIKI!!!!!

Wawa la Nyerere ndiyo chanzo.cha.mafuriko Rufiji.
 
Ili kukabiliana na athari hizi kwanza wangeweka uzio au kuta kwenye mto sehemu ambazo wao wanajua maji huwa yanatapika
Halafu pia wangejenga mabwawa makubwa kwa ajili ya maji kupungukia humo
Haya nimeyaona kwenye nchi nyingi walizotengeneza Dam
Angalia athari hiko Burkina faso Dam imejaa mito imepasuka na kusababisha mafuriko nchi ya jirani Ghana

Sasa angalia watu wa nchi nyingine wameathirika kwa uzembe wao au kutokutumia akili mwanzo au hata kuangalia watakosea wapi na wafanye nini

Hawa wasilete uswahili wameisha boronga watafute njia za kudhibiti haya maafa
Zitafutwe hela wafanye kama wengine wanavyofanya
 
Ukweli ni kuwa Tanesco wanahusika kwa 100% katika mafuriko haya yaliyoangamiza makumi ya vijiji huko Rufiji.

Kwa nini hawakufungulia maji mapema ili maji yanayokuja bwawani yahifadhiwe, badala yake wakangojea bwawa lijae ndipo wafungulie na kusababisha maji yaliyoko bwawani na maji ya mvua zinazoendelea kuvamia vijiji.

Utabiri wa hali ya hewa ulikwisha kuonyesha mvua nyingi zaidi zinakuja lakini wakakaza shingo na kufurahia kujaa maji bila kujali maafa yanayokuja.

Kwa hili lililotokea lawama zote kwa Tanesco!

Una mkataba na mvua mpaka ufungulie maji kabla ya bwawa kujaa?
 
Sasa hivi ni El Nino Bwawa limejaa kupita kiasi je wakati wa La Nina Bwawa si linaenda kukauka? Umeme wa Gesi na Upepo uboreshwe na Geo Thermal ili tusije kukwamishwa na hali ya Hewa inayopadilika kwa kasi.
 
TANESCO yasema mradi JNHPP umesaidia kupunguza athari mafuriko Rufiji,Kibiti
By Frank Monyo , Nipashe
Published at 06:43 PM Apr 11 2024

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu athari za mafuriko yanayoendelea katika maeneo ya wilaya za Rufiji na Kibiti ambayo yanahusishwa na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Kupitia taarifa yake kwa Umma, TANESCO imesema kuwa "Tunapenda kuujulisha umma kwamba uwepo wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere umesaidia kwa sehemu kubwa kupunguza athari ya mafuriko katika wilaya za Rufiji na Kibiti ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla mradi haujajengwa.

IMG-20240411-WA0015.jpg 177.89 KB

Angekuwa mwenda zake angedai bwawa ni mali japo ya jeshi la zimamoto, hadithi ikaishia hapo.
 
TANESCO yakemea upotoshaji kuhusisha mafuriko Pwani na JNHPP

DODOMA: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limefafanua kuwa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari za mafuriko katika maeneo ya Wilaya za Rufiji na Kibiti, tofauti na kinyume chake inavyoripotiwa kuwa mradi huo umechangia kutokea kwa mafuriko hayo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa TANESCO, Makao Makuu Dodoma leo imeeleza kuwa kitakwimu inaonesha kuwa maeneo ya Rufiji na Kibiti mkoani Pwani yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kwa miaka mingi ya nyuma kwa kiwango kikubwa kuliko hali ilivyo hivi sasa.

“Kama mradi wa JNHPP usingejengwa basi maji haya yangefika moja kwa moja kwenye maeneo ya Rufiji na Kibiti na hivyo kusababisha athari kubwa zaidi,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa athari za mafuriko zinazoonekana sasa zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha tangu mwaka jana hivyo kupelekea mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.

“TANESCO inakanusha taarifa zozote za upotoshaji zinazohusisha bwawa la Julisu Nyerere na mafuriko ya Kibiti na Rufiji na linakemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasio na nia njema kubeza juhuhudi za serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwa ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere,” imekemea taarifa hiyo
Naikubali taarifa rasmi
 
Back
Top Bottom