TANESCO: Watu kukaa nyumbani kipindi cha likizo chanzo cha umeme kuisha haraka

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
10,390
34,767
Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limesema kuwa limebaini mapumziko ya miezi ya Disemba na Januari ambayo watu wengi wanakuwa nyumbani katika mapumziko ya mwisho wa mwaka ndio sababu ya umeme kuisha haraka kwa watumiaji wa mita za LUKU.

Kwenye mitandao mbalimbali wananchi wanalalamika kuhusu ulaji WA umeme bila kujua kuwa tanesco wamekuja na style mpya ya kutuibia na aliyegundua hii mbinu alaaniwe Huko aliko.

20240104_162147.jpg
20240104_162136.jpg

Alhamisi, 04 Januari 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja juu ya changamoto ya usahihi wa upimaji wa matuzi ya umeme kupitia mita za LUKU.

Shirika lingependa Umma ufahamu kwamba Mita za LUKU zinazopima matumizi ya umeme kwa wateja zina ubora wa hali ya juu unaokubalika kwa viwango vya kimataifa vilivyothibitishwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).

Hata hivyo, ili kuthibitisha ubora na usahihi wa mita, Shirika linafanya uhakiki wa ufanisi wa mita kabla ya mita hizo hazijatumika kwa wateja ili kujiridhisha na viwango vya ubora.

Hali inayoendelea kwa sasa kwa baadhi ya wateja kulalamikia mita za LUKU kuonekana zinatumia umeme zaidi tofauti na matumizi yao kwa miezi ya nyuma haitokani na ubora wa LUKU hizo isipokuwa sababu mbalimbali zinaweza kuchangia ongezeko la matumizi ya umeme ikiwemo mabadiliko ya mienendo ya matumizi ya umeme kwa mwaka ambapo katika Miezi ya Disemba na Januari matumizi ya umeme majumbani huwa makubwa ukilinganisha na miezi mingine, hii inatokana na watu wengi kuwa katika mapumziko ya mwisho wa mwaka na hivyo muda mwingi kuutumia nyumbani na kupelekea matumizi mengi ya vifaa vya umeme.

Vilevile mabadiliko ya hali ya hewa yanayopelekea kuwa na ongezeko kubwa sana la joto na hivyo kupelekea wakazi wengi kutumia vipoozeo na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya umeme.

Hivyo pamoja na sababu hizo Shirika linahimiza wateja wake kuzingatia matumizi bora ya Umeme, kwa kutumia vifaa vya umeme pale tu vinapohitajika, Shirika pia, linapenda kuwakumbusha wateja wake kufanya ukaguzi wa mtandao wa nyaya za umeme ndani ya majengo yao angalau mara moja kila baada ya miaka mitano (5).

Shirika litaendelea kutoa elimu kwa wateja wake juu ya matumizi bora ya umeme mara kwa mara kupitia vyombo vya habari, mitandao yake ya kijamii na kipindi cha TANESCO NA MAENDELEO
 
Wahuni tu hawa, majuzi nimewapigia simu nikawaambia kwangu umeme umekatika wakati majirani wote wana umeme, wakaniambia kuna jirani yako anatumia umeme mwingi kwahiyo meter ya Tanesco imesense hiyo drawal ya umeme ikanikatia ili kunilinda niwe salama
 
Noma sanaa TANESCO

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ni kila mahali, ila wametoa majibu mepesi Sana kutakuwa Kuna tatizo lazima
 
Hamna shirika hapa, wtf is thi bullshit? Wako serious kweli hawa?
 
Wahuni tu hawa, majuzi nimewapigia simu nikawaambia kwangu umeme umekatika wakati majirani wote wana umeme, wakaniambia kuna jirani yako anatumia umeme mwingi kwahiyo meter ya Tanesco imesense hiyo drawal ya umeme ikanikatia ili kunilinda niwe salama
Hehehe nimecheka sana aisee kwahiyo ukawajibuje
 
kuongoza Tanzania ata ukiwa tahira unaweza kuongoza waTanzania sisi ni mazezeta kwa kweli. majibu gani hayoo Tanesco wanatoa kweli tuna safari ndefu.
 
Wahuni tu hawa, majuzi nimewapigia simu nikawaambia kwangu umeme umekatika wakati majirani wote wana umeme, wakaniambia kuna jirani yako anatumia umeme mwingi kwahiyo meter ya Tanesco imesense hiyo drawal ya umeme ikanikatia ili kunilinda niwe salama
tatizo ajira wanapeana kindugu bila kuangalia taaluma ya mtu meter zao ndio tatizo sio jirani yako nakila ikifika jioni iyo meter yako lazima ikate umeme kama sikosei
 
Back
Top Bottom