Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 478
- 690
Ni kero kutwa nzima hakuna umeme na bado usiku mnakata tena umeme na hali hii ya joto Dar es salaam. Hakuna taarifa wala nini unakuta hakuna umeme.
Mmetulaza giza usiku kuamkia leo na sasa mmekata tena umeme . Hali hii tuishi nayo mpaka lini? Mbona mvua mikoani zinanyesha Morogoro mvua kubwa tu, mpaka hata mto Ruvu umetapika. Hivi mmeshindwa toa huduma hii?
Ni aibu kwa wageni wanaokuja nchini kwa hali hii? Arusha umeme hakuna watalii wanatuona watu wa ajabu sana. Haya napiga simu zenu mlizoweka TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri hakuna hata moja inayoonyesha inafanya kazi.
Kibaya zaidi hata kituo chenu cha mawasiliano kwa mteja namba iliyopo wateja tunakatwa tofauti na BRELA ,TRA zao ni za bure 0800. Ukipiga bado unakuta nyimbo na simu haipokelewi unaambiwa subiri mpaka bundle linaisha.
Kiukweli mnaudhi mno mnafanya nchi tunaonekana wa ajabu kisa tu umeme. Hamtuonei huruma usiku joto, wezi ,kuna watu wapo kwenye mitihani.