TANESCO mbona kama siwaelewi

g vizy

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
899
982
Imepita kama wiki moja nyuma tangu nilipoenda tanesco kwa ajili ya kuwaomba waniondolee service charge kwenye mita yangu ya hapa nyumbani,walinipatia form nikazijaza baada ya kuzaja nikaacha form kwenye meza yao kwa kuwa yule aliyenipatia ile form hakuwepo alikuwa ametoka kidogo sasa hivi juzi nilipokuwa nahitaji kununua umeme kwa njia ya simu wakaniambia kuwa unahitaji kuwa na key change kwa kuwa sikujua namna ya kuzipata ikabidi niwapigie simu Tanesco

Baada ya kuwapigia nilipowaeleza tatizo langu Mara moja wakanitumia izo key change za kubadilisha mfumo wa mita kutoka kwenye service charge kuleta katika mfumo mpya kwa bahati mbaya wakati anaendelea kunitajia simu ikakatika

Nilipowapigia tena hawakupokea ikanilazimu nifunge safari mpaka tanesco walipoangalia wakagundua kweli nilikuwa nimebadilishiwa bas ikabid wanipe izo key change nkaingize kwenye mita kisha niingize namba za umeme nilionunua ila yule jamaa wa tanesco akaniambia niwe ninaweka 9200 kwa kila inapofika tarehe 12 ya kila mwezi

Mimi nkaenda zangu niliponunua umeme wa 7000 nkapata unit 59.1 tofauti na pale awali kipindi wanakata makato yao,kwa Mimi hzo unit ni nyingi sana kwa sababu siwez kutumia zaid ya unit 2 sana sana ni moja hadi moja na nusu kwa kuwa ni matumizi ya taa,TV ,boofer ,computer na sio kila siku nawasha boofer na computer hvyo naweza kumaliza mwezi Bado unit ninazo.

Cha kushangaza ni hizo 9200 za kila mwezi nalipia za nini wakati naweza kumaliza mwezi na Bado unit ninazo za kusongesha mwezi mwingine labda kama kuna mtu anaelewa kuhusu hiki ninachosema atolee ufafanuzi kidogo
NAWASILISHA WAKUU
 
Mkuu niskilize..
Ni kweli kuwa umebadilishiwa tarrif ndo kusema kwa hiyo tarrif mpya hupaswi kutumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi.Kama umeme ukaisha kabla ya tarehe ile uliyonunua awali ya kukamilisha mzunguko wa mwezi..ukinunua utauziwa kwa bei ya penati ambayo bei ya unit itakuwa ni zaudi ya hata hii ya kawaida(consider your current tarrif)

Kwa case yako:
-Kwakuwa wewe unatumia umeme kidogo,na mwezi mzunguko wa mwezi unapokamilika unakua bado una umeme,unachotakiwa kufanya ni ikifika tarehe ya kununua ununue umeme kidogo tu say wa 3500 kwa maana hiyo utapunguza kiasi cha kununua at the same time una accumulate unused units.

General rule ni kuwa ikifika ile tarehe usiache kabisa kununua umeme!
 
Una maana kwamba unaweza kununua umeme kwa gharama yoyote wa bei ya chini ya 9200 kila inapofika hyo tarehe
 
Una maana kwamba unaweza kununua umeme kwa gharama yoyote wa bei ya chini ya 9200 kila inapofika hyo tarehe
Ni kweli! isipokuwa kwa mara ya kwanza ambayo tayari umenunua.
Angalia ile risiti ulionunulia utaona service charge haipo.

CHA KUFANYA
Tazama hivyo vikodi vingine vikivyobaki jumla yake ni ngapi so ununue umeme kidogo ambao hiyo hela itakatwa na hivyo vikodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…