Tanesco kodi ya jengo imepanda?

Mburia

JF-Expert Member
Jul 15, 2022
2,310
3,368
Wanajamvi leo nimenunua umeme wa 25,000/= na makato yalikuwa kama ifuatavyo:
MAKATO

1. VAT 2,803

2. EWURA (1%) 155.74

3. REA (3%) 467.21

4. DEBT COLLECTED 6000

TOTAL 9,426

BALANCE FROM MY 25,000 = 15,574

Sasa hii 6000/= ni ile kodi ya majengo imepanda?
 
Je mwezi uliopita ulifanya manunuzi ya umeme? Ulilipa shiling ngapi kwenye kodi ya jengo?
 
Imepanda baada ya 1500 ,sasa ni 2k.hivyo wamekukata 6k sababu huenda hukununua umeme kwa miezi kadhaa.Wanatudhulumu sana hawa majitu
 
Mwezi uliopita ulilipa kodi ya jengo? Au mara ya mwisho kununua umeme ni mwezi gani?

Kodi ya jengo imepanda kutoka 1500 mwezi uliopita hadi 2000 mwezi huu ( mwaka mpya wa bajeti ya serikali ni mwezi julai).
Ngoja na wengine wachangie mada tujue shida ipo wapi..
 
Mko bzy na wasanii wa nchini na simba na yanga hamtaki kusikiliza bajeti na kuikosoa sasa unakuja kushangaa hapa.
 

Waipeleke mpaka laki moja ndio wafurahie vizuri, tamaa mbaya sana
 
Imepanda baada ya 1500 ,sasa ni 2k.hivyo wamekukata 6k sababu huenda hukununua umeme kwa miezi kadhaa.Wanatudhulumu sana hawa majitu
Kama Kila mwaka wanaipandisha walianza na buku wakaona watu kimya wakongeza jero watu kimya saivi Tena jero watu kimya. Yaani kumiliki nyumba ama mahala pa kulala nayo ulipie Ila dp world wasamehewe Kodi milele na mktaba hauna kikomo..
Yaani hii wamefanya Kama vile upo na mwanamke unapiga sound,ukishika kichwa kimya,mara bega kimya ,unashuka kifuani kimya mara unaanza ku drink 🍼.

Hivi na Kodi za madini wanazipandisha pandisha ivi ama ndio zile mwekezaji akija anapewa muda Kama miaka mitano ili ajitafute aone Kama Kuna faida ,akimaliza mitano anadai hakuna faida anauza kampuni ama kubadisha jina na anapewa mitano Tena the scheme unaendelea ivyo ivyo eternally.
 
Wawekezaji wenyewe wanalalamika all the time na watasepa, wanalalamika makodi ni mengi

Service levy, TRA, Manispaa, madini, VAT, LATRA, hata nchi zilizoendelea sidhani kama kuna tozo za namna hii

Kodi za madini zipo juu mno, kuna service levy, pia wameingiza na TRA
 
Mko bzy na wasanii wa nchini na simba na yanga hamtaki kusikiliza bajeti na kuikosoa sasa unakuja kushangaa hapa.
Nilikuwa shamba for three months ndugu yangu navuna mazao yangu.....wanasema mali utaipata shambani...

Mimi na wasanii, tena hawa hawa wa weka mate iteleze kama nyoka pangoni, au hawa wa nafukua mtaro wapi na wapi mazee? Bora hata ungeniambia wasanii wa Kenya, ambao nimeona wakipambana ku reject Finance Bill 2024 ningekuelewa lakini siyo wa hapa Bongo.

Mpira ndiyo kabisaaa nimewaachia akina Manara, Shafii Dauda na wengine.....hivi ni kweli Simba imemsajili Ronaldo na Messi?? Kuna vibarua wangu shambani walikuwa wanabishana kwelikweli kuhusu hilo hahaaaaa......
Kwanza mpira, Betting, Booxing etc ni mbinu iliyobuniwa na wajanja huko duniani ili ku distract (loose focus) kwa jamiii ili iache kufuatilia mambo ya msingi ya nchi halafu hao wajanja, politicians, wafanyabiashara wakubwa na wapiga madili makubwa waweze kupiga na kuiba bila watu kuwasumbua sumbua.....
 
Tanzania ya makodi, najiuliza hizi pesa wanazifanyia nini? Zinapelekwa wapi? Nafkiri ni Tanzania pekee inaongoza kwa makodi duniani kote.

Kweli ni wachache wataiona pepo
Hatari sana aisee yaani 25,000 wanachukua nealy 10,000/= ?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…