Kunachangamoto ya moto imekuwepo Serengeti mwezi wote wa sita na sasa hivi inaendelea hasa maeneo ya North(Kogatende) wakati huu ambapo ndio msimu wa utalii upo juu (peak)
Tunajua huwa TANAPA wanachoma kila mwaka mwezi wa tatu hadi wa tano ila baada ya mvua kuendelea hadi msimu wa utalii ukaanza; Tulitegemea kama wata amua kuchoma wangekuwa na mpango kazi pengine wachome upande mmoja na baadae upande mwingine ila sijui ni kwa kujua au kutokujua wakaamua kuchoma serengeti karibia kila pahala kwa wakati mmoja na hadi sasa mioto inaendelea... Moshi haufai; sasa sijui wanategemea watalii walio nunua safari waende wapi???
Ukiuliza unaambiwa hawachomi tena ila moto unawaka Moshi ni mzito na wageni wengi tu wanakatisha safari na kurudi makwao au pengine kwenda mahala pengine
Sijui kama TANAPA wanajua hasara wanayoleta kwa Nchi kwani hao wageni wakirudi nyumbani wanaenda kuharibu jina letu huko huku wakidai kampuni zilizo waleta ziwarudishie fedha
Kama inafaa kikosi maalumu hata cha Jeshi kingetumwa kuthibiti hali hiyo na kuhakikisha Serengeti inabahi kivutio cha utalii kama miaka yote
UKITAKA TAARIFA ZA UHAKIKA USIWAULIZE TANAPA BALI WAULIZE MAKAMPUNI YENYE CAMPS SERENGETI huko ndio utapata data ya idadi ya wageni walio katisha safari....