TANAPA wanajua moto unaowaka Serengeti unafukuza watalii?

Hassanjk

JF-Expert Member
Feb 24, 2023
246
538
Kunachangamoto ya moto imekuwepo Serengeti mwezi wote wa sita na sasa hivi inaendelea hasa maeneo ya North(Kogatende) wakati huu ambapo ndio msimu wa utalii upo juu (peak)

Tunajua huwa TANAPA wanachoma kila mwaka mwezi wa tatu hadi wa tano ila baada ya mvua kuendelea hadi msimu wa utalii ukaanza; Tulitegemea kama wata amua kuchoma wangekuwa na mpango kazi pengine wachome upande mmoja na baadae upande mwingine ila sijui ni kwa kujua au kutokujua wakaamua kuchoma serengeti karibia kila pahala kwa wakati mmoja na hadi sasa mioto inaendelea... Moshi haufai; sasa sijui wanategemea watalii walio nunua safari waende wapi???

Ukiuliza unaambiwa hawachomi tena ila moto unawaka Moshi ni mzito na wageni wengi tu wanakatisha safari na kurudi makwao au pengine kwenda mahala pengine

Sijui kama TANAPA wanajua hasara wanayoleta kwa Nchi kwani hao wageni wakirudi nyumbani wanaenda kuharibu jina letu huko huku wakidai kampuni zilizo waleta ziwarudishie fedha

Kama inafaa kikosi maalumu hata cha Jeshi kingetumwa kuthibiti hali hiyo na kuhakikisha Serengeti inabahi kivutio cha utalii kama miaka yote

UKITAKA TAARIFA ZA UHAKIKA USIWAULIZE TANAPA BALI WAULIZE MAKAMPUNI YENYE CAMPS SERENGETI huko ndio utapata data ya idadi ya wageni walio katisha safari.

Mama anahangaika kutafuta watalii wengine huku nyumbani wanawafukuza!!!!
 
sawa mtalii,tumekusikia
umeona kamoshi sehemu moja tu ya mbuga unakimbilia huku
hiyo mbuga ni kubwa sana moto hauwezi kuwaka kiasi hicho
acha uvivu peleka watalii umpande mwingine
hicho siyo kijiji
 
Usiongee kitu usichokuwa na ujuzi nacho
1. Kama mgeni amelipia kulala mahali A unafikiri ile ni guest house kuwa una amka tu asubuhi uhamie sehebu B
2. Unafikiri ni kila sehemu ya serengeti ina faa kwa game drive wakati wote?
3.?????
 
Vijana wa Tanganyika amkeni mfanye jambo, hiyo ccm itawaburuza mpaka mkome.
 
Kunachangamoto ya moto imekuwepo Serengeti mwezi wote wa sita na sasa hivi inaendelea hasa maeneo ya North(Kogatende) wakati huu ambapo ndio msimu wa utalii upo juu (peak)
Tunajua huwa TANAPA wanachoma kila mwaka mwezi wa tatu hadi wa tano ila baada ya mvua kuendelea hadi msimu wa utalii ukaanza; Tulitegemea kama wata amua kuchoma wangekuwa na mpango kazi pengine wachome upande mmoja na baadae upande mwingine ila sijui ni kwa kujua au kutokujua wakaamua kuchoma serengeti karibia kila pahala kwa wakati mmoja na hadi sasa mioto inaendelea... Moshi haufai; sasa sijui wanategemea watalii walio nunua safari waende wapi???

Ukiuliza unaambiwa hawachomi tena ila moto unawaka Moshi ni mzito na wageni wengi tu wanakatisha safari na kurudi makwao au pengine kwenda mahala pengine

Sijui kama TANAPA wanajua hasara wanayoleta kwa Nchi kwani hao wageni wakirudi nyumbani wanaenda kuharibu jina letu huko huku wakidai kampuni zilizo waleta ziwarudishie fedha
Kama inafaa kikosi maalumu hata cha Jeshi kingetumwa kuthibiti hali hiyo na kuhakikisha Serengeti inabahi kivutio cha utalii kama miaka yote
UKITAKA TAARIFA ZA UHAKIKA USIWAULIZE TANAPA BALI WAULIZE MAKAMPUNI YENYE CAMPS SERENGETI huko ndio utapata data ya idadi ya wageni walio katisha safari....
Kwa nini Tanapa wanachoma moto? Wanatambika nini?
 
Back
Top Bottom