Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 500
- 1,194
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameandaa tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari Watanzania zinazojulikana kwa jina la “Samia Kalamu Awards 2024.”
Zoezi la kutoa tuzo hizo linatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu 2024 kwa kushirikisha Wanahabari wote nchini kwa kuhusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari mosi hadi Oktoba 26, 2024 kwenye magazeti, redio, televisheni na majukwaa ya mtandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13, 2014, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Dkt Rose Reuben amebainisha sababu zilizopelekea wao kuja na tuzo hizo.
Soma Pia: Utoaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), leo September 28, 2024
Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo cha Huduma za Utangazaji kutoka TCRA, Mha. Andrew Kisaka amesema kuwa wameamua kushirikiana na TAMWA ili kuwa na mkazo wa uandishi wa makala ambazo zinahimiza na kuhamasisha maudhui ya ndani.