Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 23
- 27
Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeeleza kwamba litahakikisha usalama wa hali ya juu katika mchezo wa kombe la shirikisho Afrika (CAF) kati ya timu ya Simba ya Tanzania na AL Masry kutoka Misri.
Jeshi linawahakikishia wananchi kwamba kutakua na ukaguzi wa hali ya juu kabla ya kuingia uwanjani, na hivyo haitaruhusiwa mtu yeyote kuingia uwanjani na silaha ya aina yoyote isipokuwa baadhi ya askari wenye jukumu la usalama eneo hilo.
Jeshi limetoa wito kwa wapenda michezo wote kufuata taratibu ili kujiepusha na vitendo visivyokuwa vya kiungwana na kikanuni katika soka.