TAMISEMI yatangaza Watumishi 5,740 wamekubaliwa kuhama Serikalini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Adolf H. Ndunguru ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa Watumishi 5,740 walioomba kuhamia kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo amesema ofisi yake imefanyia kazi maombi yote ya uhamisho yaliyowasilishwa kuanzia January–July, 2023.

Amewataka Watumishi waliokuwa katika orodha ya uhamisho katika tangazo lililotolewa January 21, 2023 na hadi sasa hawajapata vibali vya uhamisho wafike kwenye ofisi za Halmashauri zao kwa kuwa vibali hivyo vimeshatumwa.

Pia amewataka Watumishi wote waliopata uhamisho wa kubadilishana kuwa hawaruhusiwi kuomba kufuta uhamisho baada ya barua za uhamisho kutoka kwani tayari mtumishi anayebadilishana Mtumishi amesharipoti katika kituo kipya cha kazi.

Ndunguru pia amewasisitiza Watumishi wote waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kwenda Ofisi ya Rais–TAMISEMI kufuata barua hizo, pia amewataka Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa vibali vya uhamisho kwa Watumishi hao waliokamilisha mchakato na kupata vibali vya uhamisho kwani uhamisho ni haki ya kila Mtumishi.

Pia Soma: TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?

TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?
 
Attachments

  • Watumishi.pdf
    1.2 MB · Views: 40
Hongera wote,hongera katibu na waziri hakika waziri mchengerwa anajari watu na ana utu sana wizara imepata mtu,japo mimi sipo kwenye mkeka ila naelewa furaha iliyopo kwa waliopata uhamisho ndoa na familia nyingi zitapona.
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Adolf H. Ndunguru ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa Watumishi 5,740 walioomba kuhamia kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo amesema ofisi yake imefanyia kazi maombi yote ya uhamisho yaliyowasilishwa kuanzia January–July, 2023.

Amewataka Watumishi waliokuwa katika orodha ya uhamisho katika tangazo lililotolewa January 21, 2023 na hadi sasa hawajapata vibali vya uhamisho wafike kwenye ofisi za Halmashauri zao kwa kuwa vibali hivyo vimeshatumwa.

Pia amewataka Watumishi wote waliopata uhamisho wa kubadilishana kuwa hawaruhusiwi kuomba kufuta uhamisho baada ya barua za uhamisho kutoka kwani tayari mtumishi anayebadilishana Mtumishi amesharipoti katika kituo kipya cha kazi.

Ndunguru pia amewasisitiza Watumishi wote waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kwenda Ofisi ya Rais–TAMISEMI kufuata barua hizo, pia amewataka Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa vibali vya uhamisho kwa Watumishi hao waliokamilisha mchakato na kupata vibali vya uhamisho kwani uhamisho ni haki ya kila Mtumishi.

Pia Soma: TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?

TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?
Utumwa utumwa tu
 
Back
Top Bottom