LGE2024 TAMISEMI yaongeza muda wa kupokea Rufaa za Wagombea wa Serikali za Mitaa, yaagiza walioenguliwa kwa kutodhaminiwa na Vyama warejeshwe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

Senior Member
Sep 21, 2024
177
568
Waziri wa TAMISEMI, Mohamedi Mchengerwa ametangaza kuongeza muda wa Kamati za rufani za Wilaya wa kupokea, kusikiliza na kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa kwa muda wa siku mbili zaidi kutoka November 13, 2024 na sasa rufaa zitapokelewa, kusikilizwa na kutolewa uamuzi hadi November 15,2024 saa 12 Jioni ambapo amewataka Wagombea wote ambao pingamizi zao hazikukubalika kuwasilisha rufaa zao mpaka November 15, 2024.

Waziri Mchengerwa amesema amechukua hatua hiyo kufuatia maoni mbalimbali waliyoyapokea kutoka kwa Wadau wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa vikiwemo Vyama vya siasa kuhusu mchakato wa uteuzi na ushughulikiaji wa pingamizi za Wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muda wa kuwasilisha na kutoa maamuzi ya rufaa za wagombea ambao hawakuteuliwa,.

“Ninazielekeza kamati za rufani za Wilaya kuitisha fomu za Wagombea wote walioenguliwa/hawakuteuliwa ili kufanya mapitio na kujiridhisha na sababu zilizopelekea Wagombea hao kutoteuliwa ili haki iweze kutendeka kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi, ninawaelekeza Wasimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri zote kuwarejesha

Soma Pia:

Wagombea wa Vyama vyote ambao walienguliwa kwa sababu ya kutodhaminiwa na Vyama vyao katika ngazi ya Kijiji/Mtaa pamoja na kuwa Vyama hivyo viliwasilisha barua za kuainisha gazi ya chini ya udhamni kuwa ni Kata ikiwemo Chama chanACT-Wazalendo kilichowasilisha ngazi yake ya udhamini kuwa ni ngazi ya Kata”

“Ninavihimiza Vyama vya siasa ambavyo Wagombea wao wameenguliwa kutumia vizuri muda huu wa siku mbili ulioongezwa endapo hawakuridhika na uamuzi wa Wasimamizi wasaidizi kuhakikisha wanasimamia Wagombea wao wawezenkuwasilisha rufaa zao kwa kamati za rufani zilizopo katika kila wilaya husika”

TAMISEMI
Snapinsta.app_466324027_18352435804193701_7659952039828760736_n_1080.jpg
Snapinsta.app_466528893_18352435813193701_6001555462692458886_n_1080.jpg
 
Sasa tumerudi nyuma sana zamani haikuwa hivi kwenye mambo ya uchaguzi. Tuliuheshimu lakini sasa lakini sasa katibu nini sijui huko katani anathubutu tuu kumjazia mtu mlemavu.
 
Waziri wa TAMISEMI, Mohamedi Mchengerwa ametangaza kuongeza muda wa Kamati za rufani za Wilaya wa kupokea, kusikiliza na kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa kwa muda wa siku mbili zaidi kutoka November 13, 2024 na sasa rufaa zitapokelewa, kusikilizwa na kutolewa uamuzi hadi November 15,2024 saa 12 Jioni ambapo amewataka Wagombea wote ambao pingamizi zao hazikukubalika kuwasilisha rufaa zao mpaka November 15, 2024.

Waziri Mchengerwa amesema amechukua hatua hiyo kufuatia maoni mbalimbali waliyoyapokea kutoka kwa Wadau wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa vikiwemo Vyama vya siasa kuhusu mchakato wa uteuzi na ushughulikiaji wa pingamizi za Wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muda wa kuwasilisha na kutoa maamuzi ya rufaa za wagombea ambao hawakuteuliwa,.

“Ninazielekeza kamati za rufani za Wilaya kuitisha fomu za Wagombea wote walioenguliwa/hawakuteuliwa ili kufanya mapitio na kujiridhisha na sababu zilizopelekea Wagombea hao kutoteuliwa ili haki iweze kutendeka kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi, ninawaelekeza Wasimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri zote kuwarejesha

Soma Pia:

Wagombea wa Vyama vyote ambao walienguliwa kwa sababu ya kutodhaminiwa na Vyama vyao katika ngazi ya Kijiji/Mtaa pamoja na kuwa Vyama hivyo viliwasilisha barua za kuainisha gazi ya chini ya udhamni kuwa ni Kata ikiwemo Chama chanACT-Wazalendo kilichowasilisha ngazi yake ya udhamini kuwa ni ngazi ya Kata”

“Ninavihimiza Vyama vya siasa ambavyo Wagombea wao wameenguliwa kutumia vizuri muda huu wa siku mbili ulioongezwa endapo hawakuridhika na uamuzi wa Wasimamizi wasaidizi kuhakikisha wanasimamia Wagombea wao wawezenkuwasilisha rufaa zao kwa kamati za rufani zilizopo katika kila wilaya husika”

TAMISEMI
View attachment 3150871View attachment 3150870

Hadi CCM iseme ndipo watu watendewe haki.
Safari bado ni ndefu sana.
 
Kwa sasa nashauri vyama vya upinzani kuachana na mapingamizi, hawa walidhamilia kutumia fedha za umma na wakijua hawako tiyari kwenda kwenye uchaguzi.
Ushauri wagombea wote warudishwe kura za wananchi ziseme au

Mchakato uanze upya na Mchengerwa alipe izo gharama( naungana na lissu)
 
Back
Top Bottom