Bima ni mkataba wa kulipa fedha katika shirika la fedha ili kupata fidia wakati mlipaji anapofikwa na ajali au hasara fulani au kurejeshewa fedha zake pamoja na faida baada ya muda maalumu.
fahadykimaro@gmail.com
- Bima ya gari hutosheleza gharama ya gari lako kama likiharibika au likiibiwa.
- Bima ya nyumba (bima ya ujenzi) hutosheleza gharama ya kubadilisha vitu kama kukitokea kitu nyumbani (kwa mfano, uharibifu kutoka moto au kimbunga).
- Bima ya vitu vya ndani hutosheleza gharama ya kubadilisha au kutengeneza vitu ulivyo navyo nyumbani kama fenicha, nguo, chombo cha kufanyia kazi na mapambo ya vito.
- Bima ya maisha hulipia kiasi cha pesa kilichoteuliwa wakati unapokufa. Pesa hizi huenda kwa watu unaochagua wapokee pesa hizo (hii imeandikwa kwenye hati yako ya bima).
- Bima ya usafiri hutosheleza gharama ya vitu fulani kama ukipata shida wakati uko mbali na nyumbani. Kwa mfano: kama ukiwa mgonjwa au ukiumia na kupata matibabu ya dawa; kama ukipoteza kitu na ulazimike kukibadilisha; kama kitu chako kikiibiwa na unahitaji kukibadilisha; au kama mipango yako ya usafiri ikibadilika (kwa mfano, safari yako ya ndege ikifutiliwa mbali).
- Bima ya afya hutosheleza kiasi fulani cha gharama ya matibabu ya dawa kama ukigonjeka au ukiumia.
- Bima ya simu ya mkono hutosheleza gharama ya vitu vingine ambazo zinaweza kufanyika kwenye simu yako (Kwa mfano, kama ikiwacha kufanya kazi au ukiiharibu)
- Chagua kampuni bora ya Bima hapa unaweza fanya uchunguzi mwenyewe au kwa msaada wa broker au agent
- Fanya kukata bima katika agent au Broker kwa sababu hawa wapo kuhakikisha maslai ya mteja yanatimizwa kwa ufasaha.
- Soma mkataba vizuri na kuelewa
- Pata msaada kwa kuelewa juu ya nini cha kufanya pindi unapata majanga
fahadykimaro@gmail.com