Tamasha kubwa litakalojulikana kwa jina la Wavuvi Festival &Culture Tourism Tanzania liko njiani kufanyika kwa siku mfululizo jijini Dar es Salaam likiwa ni la kwanza katika historia ya nchi.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Alphone Mkama, Wavuvi Festival litafanyika kwenye Ufukwe wa Coco (Coco Beach), Juni mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan.
“Ni tamasha la aina yake kwa kweli. haijawahi kutokea kwa Tanzania. Lengo la tamasha hili ni kukusanya fedha, kiasi cha shilingi milioni mia nne na hamsini (450,000,000) ili kununua boti ziendazo kasi kwa ajili ya kuwaokoa wavuvi punde wapatapo ajali baharini na kupoteza maisha kwa sababu ya kukosa uokozi wa haraka.
“Wengi hawajuhi, wavuvi huwa katika hatari kubwa wanapokuwa baharini wakivua samaki. wakipata ajali, hakuna boti ya kasi ya kwenda kuwaokoa. Kwa hiyo tunataka kununua bosti tatu, kwa ajili ya Dar, Mtwara na Mafia,” alisema Mkama.
Akaongeza: “Mambo yote ya kulifanya tamasha liwe halali yamekamilika. Kwa sasa tunaweka kamati sawasawa sambamba na kutafuta wadhamini ambao watashirikiana na tamasha hili la siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi.”
Pia Mkama alisema kuwa, siku hio katika tamasha kutakuwa na burudani mbalimbali, nyama choma, mbuzi choma, kuku choma na samaki choma kwa wingi. Lakini pia, alisema makampuni na watu binafsi ambao watataka kuchoma nyama na kuuza vinywaji wanakaribishwa kwa mazungumzo.