Takwimu za Mawasiliano Robo ya Mwaka inayoishia Juni 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,739
13,502
Ripoti hii inawasilisha takwimu za mawasiliano za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024. Kwa ujumla, ripoti inatoa takwimu za mawasiliano ya simu, pesa mtandao, Intaneti, utangazaji, posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto, na huduma nyingine zinazohusiana na teknolojia ya Habari na mawasiliano kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Takwimu zimeandaliwa kulingana na viwango vya Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) vya kukusanya na kuandaa takwimu za huduma za mawasiliano/TEHAMA.

Takwimu za usajili wa laini za simu
Laini za simu za mkononi na za mezani ambazo zimetumika angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita zinaonesha kuna ongezeko la Asilimia 4.3 kwa Laini zilizosajiliwa.

Kuna aina mbili za laini, kwanza ni zile zinazotumika kwa mawasiliano ya binadamu (Person to Person - P2P), nyingine ni zinazotumika kwa mawasiliano ya mashine (Machine to Machine - M2M).

Laini za Simu zilizosajiliwa Machi - Juni 2024 ni Milioni 73.4 hadi Milioni 76.6

Laini zote (P2P na M2M)
Kufikia Machi 2024
Laini Milioni 73.4

Kufikia Juni 2024
Laini Milioni 76.6
Ongezeko 4.3%

Usajili wa Laini za P2P (Mtu kwa Mtu)
Kufikia Machi 2024
Laini Milioni 72.5

Kufikia Juni 2024
Laini Milioni 75.6
Ongezeko 4.3%

Usajili wa Laini za M2M (Mashine kwa Mashine)
Kufikia Machi 2024
Milioni 0.93

Kufikia Juni 2024
Milioni 0.97
Ongezeko 4.3%

Idadi ya laini za simu za mkononi na mezani za mawasiliano ya binadamu (Person to Person - P2P) zilizosajiliwa kwa kila mtoa huduma April ilikuwa 72,615,633, Mei 73,800,712 na Juni ni 75,588,006

Takwimu hizo ni kwa mitandao ya Simu ya Airtel, Halotel Tigo, TTCL na Vodacom ambapo zinaonesha ongezeko la wastani la kila mwezi la 2% la usajili ndani ya Robo ya Mwaka iliyoishia Juni 2024

Line za simu.jpg


Mgawanyo wa Usajili wa Laini za Simu kwa kila mtoa huduma

Takwimu za laini za simu za mkononi na mezani za mawasiliano ya binadamu (Person to Person - P2P) zinaonesha kuwa hakuna mtoa huduma aliyezidi 35%, ambayo ni kiwango cha chini cha umiliki wa soko, hii inaonesha kuna ushindani wenye tija kati ya watoa huduma.

Hata hivyo, kwa usajili wa mawasiliano ya mashine (Machine to Machine - M2M), Vodacom ana 56.9% ya laini zote zilizosajiliwa, Airtel inashika nafasi ya pili kwa 34.0%, ikifuatiwa na Halotel kwa 5.9%
Screenshot 2024-07-23 150242.jpg



Dar inaongoza kwa kuwa Laini nyingi za Simu
Tanzania Bara
Dar Laini.jpg


Bei (Tsh) ya kupiga simu ndani na nje ya Nchi bila kifurushi
Bei za huduma ya sauti kwa Robo ya Mwaka inayoishia Juni 2024 kwa simu za ndani na nje ya nchi Imeonesha Watoa Huduma wote hutoza Tsh. 30 kwa dakika moja ndani na nje ya mtandao, isipokuwa Halotel inayotoza Tsh 10 kwa dakika moja ndani ya Mtandao na Tsh 20 nje ya Mtandao.

Hiyo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Huduma za Mawasiliano ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo bei hizo ni za sauti kwa dakika moja wakati Mtumiaji anapiga simu ya ndani au ya kimataifa bila kujisajili kwenye kifurushi

Pia, wastani wa bei ya huduma ya sauti kwa dakika moja kwa Afrika Mashariki na Nchi nyingine ni Tsh 713.16 na 1,869.45, mtawalia.
Screenshot 2024-07-25 124033.jpg
 
Back
Top Bottom