TAKE ONE YA CLOUDS TV NA MUENDELEZO WA MAKOSA YALE YALE

y-n

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,389
2,510
Wadau,nimeangalia kipindi cha jumenne hii (tar9/Aug2016) cha TAKE ONE AND ACTION cha CLOUDS TV kinachoendeshwa na ZAMARADI MKETEMA na kwa mawazo yangu naona bado kipindi kina muelekeo wa kurudia makosa yale yale yaliyosababisha wapewe sijui ni onyo na TCRA.
Zamaradi,(Muendesha kipindi) alimuhoji dada mmoja anajiita GIGY MONEY lakini maelezo yake ndio yanayonitatisha.
Kwa mtazamo wangu mimi naona mahojiano yale bado hayakuwa mazuri kimaadili maana alichokizungumzia ni kuweka wazi mambo ya mahusiano yake hadharani na huku akionesha ni namna gani alivyoweza kupata faida mbalimbali na mahusiano yale.
Amewataja hadharani watu mbalimbali alio-date nao kitu ambacho nadhani sio kizuri kimaadili.
Swali langu ni je?hivi ni lazima Zamaradi ahoji maswali ya aina ambayo yatamfanya mtu atoke nje ya maadili ya jamii??
Nini mtazamo wenu wadau wengine ambao mlikiangalia kile kipindi??

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom