KERO Taka zinazagaa ovyo Mtaa wa Nyabulogoya, Nyegezi (Mwanza), kifaa cha kutupia taka nacho ni taka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
204
246
WhatsApp Image 2024-12-01 at 18.52.18_5f37e021.jpg
Sisi Wananchi wa Mtaa wa Nyabulogoya, Kata ya Nyegezi tuna changamoto ya kukosekana kwa chombo imara cha kuweka taka katika maeneo yetu licha ya kuwa tumekuwa tukitoa taarifa kwa Mamlaka zinazohusika juu ya hali hiyo.

Kifaa kilichopo kimechoka na hakifai, hata chenyewe ni sehemu ya takataka pia kwa sasa.

Matokeo yake watu wengi hasa wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani wamekuwa wakilazimu kutupa takataka Kando ya Barabara na hivyo kusababisha taka kuzagaa ovyo.

Viongozi wetu wa Serikali ya Mtaa wanajua kila kinachoendelea lakini kama nilivyosema hawajayafanyia kazi.

IMG_20241202_104024_977.jpg

WhatsApp Image 2024-12-01 at 18.52.18_e4d70a35.jpg
 
Back
Top Bottom