Taifa limepoteza muelekeo, binti aliyepotea anasakwa na vyombo vya usalama vya nchi mzima huku Dp world wakipigiwa debe kwa nguvu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,241
4,811
Kwa hiyo siku hizi vyombo vya usalama ndani ya kata, wilaya na mkoa haviwezi kufanya majukumu yao? Kwa ishu ndogo kama kupotea mwanafunzi

Msukuma amegeuka kuwa mpiga debe wa Dp world

Watu wanasahah mambo ya msingi kama kujadili bajeti.

Alafu tunaambiwa Mwigulu ni waziri bora hajawahi kutokea.
 
Hii issue ya huyu dogo ina dots nyingi ambazo haziungi. Haiwezekani upuuzi kama huo uwe mjadala wa kitaifa.
Ilikuwa ni diversion kutoka njia kuu ya DP world.

CCM na serikali daima huwa na policy moja ya kutengeneza tatizo na kisha kujifanya kutoa suluhisho la hilo tatizo.

Kwa Esther walibugi maana sasa hivi tofauti na enzi za makaa ya mawe, kuna teknolojia ambayo inafanya taarifa kusambaa haraka.
 
Ilikuwa ni diversion kutoka njia kuu ya DP world.

CCM na serikali daima huwa na polisi moja ya kutengeneza tatizo na kisha kujifanya kutoa suluhisho la hilo tatizo.

Kwa Esther walibugi maana sasa hivi tofauti na enzi za makaa ya mawe, kuna teknolojia ambayo inafanya taarifa kusambaa haraka.
Ndio kawaida maana hii nchi tulishazoea kuyumbishwa na kiki za kijinga.

Huwa mara zote ikiibuka issue sensitive lazima baada ya hapo uibuke utopolo wa kuwapoteza raia maboya na huwa tunakimbilia huko kama manyumbu.
 
Kwa hiyo siku hizi vyombo vya usalama ndani ya kata, wilaya na mkoa haviwezi kufanya majukumu yao? Kwa ishu ndogo kama kupotea mwanafunzi

Msukuma amegeuka kuwa mpiga debe wa Dp world

Watu wanasahah mambo ya msingi kama kujadili bajeti.

Alafu tunaambiwa Mwigulu ni waziri bora hajawahi kutokea.
Sasa hapa unajadilia hoja gani mbona Haina miguu?
 
Kwa hiyo siku hizi vyombo vya usalama ndani ya kata, wilaya na mkoa haviwezi kufanya majukumu yao? Kwa ishu ndogo kama kupotea mwanafunzi

Msukuma amegeuka kuwa mpiga debe wa Dp world

Watu wanasahah mambo ya msingi kama kujadili bajeti.

Alafu tunaambiwa Mwigulu ni waziri bora hajawahi kutokea.
Wanatuambia Kuna majizi bandari police wameshindwa kuyakamata wakaona dawa nikuuza bandari zetu ili kuwakoma majizi hao.
 
Huyo binti ni wale mabinti waliowekewa kanuni ya kuolewa hata kabla ya kufika miaka 18.

Ukitazama shule wanamlazimisha sana na yeye ameshakuwa matured anajua anachokitaka. Why wanamlazimisha abakie shule na hataki?!

Hapo watatafuta tu matatizo hili swala lingetatuliwa ngazi ya familia sio shule wala serikalini.

Mabinti wa namna hii wapo wengi sana hawafanyi maamuzi kwa shinikizo la wazazi wala nini ni maamuzi yao binafsi kuamua kuolewa na kuanza maisha katika umri huo wa kupevuka. Na wengine huwa wanatoboa bila shida hadi utu uzima.

Kuna hii tafsiri kuwa kila binti anataka kuolewa basi anakwenda kuharibu maisha yake huu sio ukweli wa uhalisia wa kimaisha kwasababu itategemea anakwenda kufanya maisha wapi na anakutana na nani.

Mbona huwa hatuzungumzii maisha ya mabinti waliokwenda shule hadi kufika chuo kikuu, na wakamaliza salama, ila wakarejea mtaani hawana maisha ya kueleweka, hawana wanaume wa ndoa, hawana watoto au wanaamua kuzalia nyumbani, wanaishi maisha ya kuunga unga.

Why hawa hatuongelei jamii inakaa kimya tunajaribu kusema nini sasa hapo kwamba kufanikiwa kwa binti ni kuwa na elimu makaratasi ambayo haitumii popote inabakia kuwa ni decoration anabakia kutangatanga huku vijana ambao walikuwa stahiki yake wakiwa wameshapata wenza na kuanza maisha ya ndoa na kujijenga kiuchumi na wenza wao.

Hapa me nadhani tunalazimisha watoto wa watu kubet na maisha yao. Kama mtu anaona ana maisha nje ya shule ni vema akaachwa especially mtoto wa kike maana asikwambie mtu mtoto wa kike akikaa mwaka m'moja unaisha hakuna jambo la maana kafanya hasara yake ni sawa na kampuni kuwaweka wafanyakazi site huku kazi zimesimama kwa mwezi mzima huku kila wakienda wanagharamikiwa chakula, malazi na posho daily.
 
Back
Top Bottom