Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Wadau nimeamua kuweka habari hii kuwapa taadhari vijana wapya wanaotaka kujiingiza kwenye kilimo. Kuna usemi unaosema kwamba kupitia failure ndio kujifunza, huo usemi uko sahihi, lakini kupitia kwa aliefail kujifunza inasaidia sana. Mimi ni moja ya watu waliopata hasara kupitia kilimo. Nataka wewe mkulima mpya au uliekosea kwenye kilimo uweze kuwa makini ili upate tija katika kilimo
Watu wengi wamekuwa wakidanganywa kwamba kwenye kilimo pesa iko nje nje, ni kweli kuna pesa nyingi lakini si rahisi kama watu wanavyodhani. Kwa bahati mbaya wakulima huwa hawasemi ukweli, unaweza kukutana na mkulima akakwambia kila mwaka analima ekali 10 za mahindi na anavuna gunia 150 hadi 200. Hivyo ukipiga bei kwa haraka haraka unaweza ukwamwambia nitafutie ekari 20 na mimi nilime ili nipate gunia 400.
Utakapo hamua kulima utakuta hali ni tofauti kabisa maana kuna changamoto zifuatazo ambazo ni lazima uzikabili:
1. Kwa sasa kuna tatizo kubwa la ukame, yaani unapanda mazao yako lakini mwisho wa siku yanakauka au yanakuwa hayana afya nzuri, hii usababisha mavuno kidogo. Kulima kwa kutegemea mvua ni mchezo wa kubahatisha
2. Wengi tumezoea kulima kienyeji, yaani hatupimi PH ya udongo, pia hatuweki mbolea.
3.Kuna changamoto kubwa kwa upande wa upandaji, wengi tunapanda lakini hatupandi kwa population inayotakiwa. Unaweka vibarua wapande, lakini space kati ya mmea na mmea inakuwa siyo sahihi. Hivyo unaweza kusema kuwa mwaka huu umelima ekari 40 lakini kwa uhalisia ni ekari 25 kwa sababu ya space kuwa kubwa.
4.Usimamizi. Kwa wale walioajiriwa hii ni changamoto kubwa sana, kilimo cha kupiga simu ni hatari. Mara nyingi msimamizi wako atakwambia mazao yako vizuri, lakini ukienda shambani unakuta ni tofauti kabisa, unaweza kupata presha. Pia unaweza kutuma pesa lakini isifike shambani, matokeo yake msimamizi anatumia kwa matumizi yake mwenyewe na kuwalipa vibarua akiwa amechelewa
5. Mavuno. Moja ya changamoto ya mkulima ni bei ya mazao, wakati wa mavuno mazao ushuka bei, hapa lazima utafute mahali pa kuhifadhi mazao yako hadi soko liwe imara.
NB: Uzi huu ni kwa ajili ya kukusaidia wewe usie na uzoefu ili usije ukakurupuka, wala siyo kukukatisha tamaa, ni vyema ukajua changamoto hizo ili uweze kupata matokeo mazuri utakapo hamua kulima kwa umakini.
Ili upate gunia 20 za mahindi kwa ekari moja ni lazima uwe umefanya intensive care ikiwemo kumwagilia, bahati mbaya mabwana shamba na wauza mbegu huwa wanadanganya wakulima kuhusu uzalishaji kwa ekari moja.