Tahadhari kipindi cha mvua

TANESCO

Official Account
Jul 12, 2014
4,595
2,115
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa tahadhari kwa wateja wake kuzingatia yafuatayo kipindi hiki cha mvua nyingi

1.Kutoa taarifa mapema mara inapotekea hitilafu yeyote kwenye miundombinu ya umeme kulikosababishwa na mvua au sababu nyingine.

2.Kutokukaa au kufanya shughuli yeyote chini ya miundombinu ya umeme.

3.Kutoa taarifa mapema maeneo yenye mafuriko au mkusanyiko wa maji mengi ili kusadia kuchukua tahadhari

4. Endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi ukawekwa kuzuia wapita njia na watoto kuathirika

Shirika linawamba radhi wateja wake wa maeneo mbalimbali ambao wametoa taarifa na wataalamu wetu kuchelewa kufika, Hii inatokana na ugumu uliopo wa kupita baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua,

TANESCO tunayaangaza maisha yako

Imetolewa na :
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
Umeme umecheza kweli huku kwetu hadi taa yangu ikaungua... Nilichelewa kuizima
 
Reactions: BAK
Eneo gani na namba yako ya simu
Hivi jamani kwa wilaya ya mkuranga kuna tatizo gani hasa kwenye kuunganishiwa umeme?!! Hivi hili zoezi la kusambaza nguzo linaloendelea sasa hivi ni kwa maombi ya mwezi wa ngapi? Kwani kila siku ukienda unapewa majibu tofauti tofauti kutegemea na mtu unayekutana naye ofisini siku hiyo?!! Mimi toka january 9,mwaka huu nimelipia hadi leo. Nikienda sipewi jibu moja la kujitoshereza. Labda naweza pata jibu toka kwenu leo hii kwani ukiangalia kwenye kumbukumbu zenu nimeshawapa particulars zangu zote kupitia hapa jf!! Ila hadi leo kimya hamtutendei haki!! Feed back ni mhimu ili mteja ajue kuwa suala lake linafanyiwa kazi.
 
Nenda Pale Mkulanga Kaonane na mtu Mmoja iv Anaitwa Mvungi Yeye ni Meneja wa kituo Icho Ukifka mueleze shida zako
 
Dah...kweli Karumekenge technique imefanya kazi......Hata nyinyi TANESCO
 
Kipindi hiki cha mvua huwa ni hatari hasa kwa watoto. Nguzo nyingi na nyaya huanguka, watoto elimu ya usalama hawana kabisa na kujikuta wakipoteza maisha.
 
Asante mdau ningependa kuuliza je kama eneo mlilofunga mita pale mlipopitisha mstimu wenu mvua ikinyesha kubwa huwa panatiririsha maji ila miter ipo kwenye kibox je inaweza leta short?
 
4. Endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi ukawekwa kuzuia wapita njia na watoto kuathirika


Kuna kiongozi wa serikali ya mtaa amefikisha taarifa Tanesco kuwa kuna nguzo imeng'olewa kizuizi kwa makusudi na mtu ili kupitisha ukuta wa nyumba yake, na sasa nguzo hiyo inakaribia kuanguka lakini yapata mwezi na nusu Tanesco hawajachukua hatua, kwa maana hiyo inaonekana Tanesco mnawapotezea muda watoa taarifa kwakuwa hamfanyii kazi taarifa wanazowapa
 
Wamesahau kukumbusha wateja wao kuhakikisha kuwa wanzima fridge wanapotoka
majumbani mwao , maana hili suala la kata washa... kata ...washa ...umeme linaweza zua kizaaa
zaa cha majanga.

 
Ila kwetu mbagara Kirungure na njia ya chamazi mbandekwa nini siku ya Jumamosi lazima umeme unakuwa hakuna ikifika saa 8:00AM why huwa nashangaa sana, mda mwingine ata katikati ya wiki unakatika hautabiliki na haunaga taarifa. Mtusaidie kwa kweli vituvyetu vinaharibika sana kwenye mafriji hasa kwa sisi wenye watoto na atushindi nyumbani.
 
Tunaomba taarufa zifuatazo
eneo gani
namba ya simu
namba ya taarifa aliyopewa
 
Mbezi beach b maeneo ya shoppers kuelekea makonde umeme ulipungua jioni na sasa umezima kabisa. Tafadhali shughulikieni
 
Tunaomba taarufa zifuatazo
eneo gani
namba ya simu
namba ya taarifa aliyopewa


Ingependeza kama ingekuwepo central number ambayo issues zote zinaripotiwa kupitia namba hiyo, halafu hawa wa mikoani wanapewa maagizo na ninyi makao makuu, then ninyi mnawasiliana na watoa taarifa kujua kama marekebisho yamefanyiwa kazi, uzoefu wetu ni kuwa Tanesco mikoani ni wapuuziaji, hawafanyii kazi taarifa za wananchi, nina mifano halisi mingi ya nguzo na waya hatarishi katika eneo hilo, kama mngeweza nendeni mkakague line zote za umeme zilizo karibu na makazi ya watu mtaona waya zingine zipo mita 3 toka ardhini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…