Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 262
- 466
Nimeona mabango na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na pia nimepita maeneo ya Kawe Tanganyika Packers na viunga vyake naona watu wameanza kumiminika ikiwa ni maandalizi kuelekea mkubwa mkesha mkubwa uliopewa jina la " 'MKESHA USIO SAHAULIKA' CHAKO NI CHAKO" ambapo unatarajia kufanyika kesho Julai 05/07/2024.
Kwa hali na mazingira yalivyo inaonesha kutakuwepo na kundi kubwa la Watu ambao wanatarajiwa kufika eneo hilo kutoka mikoa mbalimbali hata nje ya Nchi huku wengine wakiwa tayari wameanza kuwasili kwenye viwanja hivyo.
Ambapo nilipopita eneo hilo wengine nimeona wakiwa na Watoto wadogo jambo ambalo linanipa hofu hasa usalama wa watoto hao endapo watu watakuwa wengi zaidi.
Niliposikia kutakuwepo na zoezi la kukanyaga mafuta imenifanya kurejesha kumbukumbu zangu nyuma na kukumbuka tukio la mwaka 2020 watu wasiopungua 20 walidaiwa kufariki dunia kwenye viwanja vya Majengo Mjini Moshi wakati zoezi la kukanyaga 'Mafuta Upako' kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa.
Uenda ni mashaka yangu lakini natahadharisha umma ambao unapanga kwenda eneo hilo kuzingatia usalama binafsi ikizingatiwa mkesha huo unaanza majira ya saa mbili usiku hadi asubuhi saa 12 asubuhi.
Pia nitoe wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutia jicho la tatu kwenye mkesha huo na lolote hasi hasa linalohusu usalama wa raia ambalo likitokea wahusika wawe tayari kuwajibika au kuwajibisha watakaopelekea changamoto endapo ikijitokeza.