Tahadhari: Horn of Africa Aid Relief ni NGO ya kitapeli

Cruzoo

Member
Jan 30, 2014
37
17
Salam sana wakuu.

Kuna NGO inayoitwa jina hilo hapo juu, Walitangaza kazi zenye mishahara mizuri sana kuanzia Dola 4700+ kupitia website yao na pia tangazo liliwekwa zoom Tanzania. (Careers Vacancies- Horn of Africa Aid)

Naweza kuthibitisha pasipo na shaka kuwa hii NGO haipo, na HR Manager wao anayejiita HAZEL CLOE naye ni tapeli pia. Wameshatapeli watu wengi sana kupitia wizi wa namna hii kwa kufanyishwa GPS Test etc.

Nitajazia maelezo ya ziada baadae. Ila kwa yeyote aliyeomba kazi kwenye NGO hio au anayetakiwa kufanya GPS Test kwa hawa wanaoitwa FAVRAN AFRICA (wapo Kenya kupitia jamaa anayeitwa DENA SANGA) Tafadhali sitisha mpango wako.

Wasalaam,

Cruzoo
 
Mheshimiwa niliponea chupuchupu...mahali nilipowagundua nikawaambia sina uwezo wa kulipia GPS kama vp wanisaidie then wanikate kwenye salari..hadi leo nikituma email kwao hazijibiwi tenaaa!!!!!!
 
duh! hiyo gps test ndo inakuwaje ss? haya mambo ya kazi ukiambiwa ulipie chochote ht km ni cha buku 2 ujue apo utapeli tuu.
 
Asante kwa Taarifa mkuu
Sasa mkuu mbali nakuandika hapa umechukua hatua gani kama wewe binafsi.
Hembu wasiliana na TAKUKURU pia nenda Brella kama usajili upo na sehem zoote wanazotoa vilabi kwa Taasisi hizo.
Kisha wafikishie na Polisi wafanye yao
 
Back
Top Bottom