DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Ngao One

Member
Jan 26, 2011
35
29
1111.jpg

UPDATE: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule ametembelea Mtaa wa Nia Njema Mei 23, 2023, baada ya kusoma post hii ya JF

DC aliambatana na Mhandisi wa Wilaya na maafisa wengine. Baada ya kukagua ujenzi wa gorofa hilo, wamebaini kuwa linajengwa bila kibali cha manispaa na chini ya kiwango, hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi

DC ameagiza kiongozi wa serikali ya mtaa awekwe ndani kwa kushindwa kuchukua hatua

Pia DC amempa siku 1 afisa wa TRA anayemiliki jengo hilo aripoti ofisi yake

Wakazi wa Mtaa wa Nia Njema, Mbezi Juu, wanaishukuru JF kwa kusaidia malalamiko yao yamfikie DC na hatua kuchukuliwa kusitisha ujenzi wa gorofa hilo hatarishi

Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
 
Attachments

  • 2222.jpg
    2222.jpg
    70.8 KB · Views: 55
Afisa wa TRA mwenye uwezo wa kujenga ghorofa 4 mshahara wake ni tsh ngapi ?.Au ndio wale wa kubambika kodi kubwa kubwa halafu baada ya kushindwa kulipa mnakaa kitako mnazungumza.

Kodi zinatakiwa kueleweka vizuri mfano kodi za magari ukinunua gari aina fulani ya mwaa fulani kodi yake ipo wazi.Ukileta kontena 40ft kodi yake mazungumzo.

Hawa akina Bon tutawazalisha kweli kweli kama tunavyowazalisha matrafic wala rushwa kwa kushindwa kuweka mifumo mizuri barabarani.
 
Bwana Mdogo anasagiwa kunguni hyo inaitwa usianzishe ugomvi wa mawe Kama unaishi kwenye nyumba yenye vioo.

Mzaramo anakwambia hukuja kwenye arobain ya mwanangu namie siji kwenye msiba wa baba yako.

Weka ugoko niweke chuma tuone Nan ataumia.
 
Afisa wa TRA mwenye uwezo wa kujenga ghorofa 4 mshahara wake ni tsh ngapi ?.Au ndio wale wa kubambika kodi kubwa kubwa halafu baada ya kushindwa kulipa mnakaa kitako mnazungumza.

Kodi zinatakiwa kueleweka vizuri mfano kodi za magari ukinunua gari aina fulani ya mwaa fulani kodi yake ipo wazi.Ukileta kontena 40ft kodi yake mazungumzo.

Hawa akina Bon tutawazalisha kweli kweli kama tunavyowazalisha matrafic wala rushwa kwa kushindwa kuweka mifumo mizuri barabarani.
Kwamba yeye kwao ni masikini?
 
Dawa ni kusomea uhasibu au kodi kwa gharama yoyote . Utumishi ajira za tra zinatangazwa kila baada ya muda mfupi na wala hazina ugumu.
Sema maskini wengi waoga hukimbilia ualimu na udaktari ili wakashike maiti.
Hata mashamba ya ukoo uza jisomeshe au somesha mtoto
Kwa hiyo waliosomea uhasibu na mambo ya kodi wote wameajiriwa mzee......
 
Kwamba yeye kwao ni masikini?
Ulishawahi kuona mtoto wa bilionea anaajiriwa hovyo hovyo ?.

Ukiuliza huyo Bon anafanya biashara gani na analipa kodi iasi gani utabaki kushangaa na kusikitika.
Leo hii hakuna trafic asiyekuwa na usafiri wa uhakika,nyumba nzuri kwasababu ya rushwa za barabarani,jiulize kwanini askari anyelinda bank hana hata baskeli !.

Nchi yetu inahitaji viongozi watakao kuwa tayari kupambana na mifumo ya rushwa.
 
Nimekuuliza swali hujajibu
 
Back
Top Bottom