Kwa kweli ni ngumu sana kuelewa dhamira ya kilanja, unapowachukia matajiri kwa kudhani unawasaidia masikini matokeo yake ndio haya tunayokumbana nayo, matajiri wamebaki na utajiri wao ile pesa waliokuwa wameiweka kwenye mzunguuko wameitoa hawana hakika ya kesho kilanja ataongea nini, tumebaki tunashangaa, kilanja alipotishia atabadili fedha wakanunua hela ya malkia na ya George Washington hali ni tete madeni hayalipiki baadhi tumepoteza nyumba ukipata leo unashukuru hujui kesho utakula nini, kifupi tumerudi miaka 20 nyuma, ya Mkapa na Kikwete yote yanapotea, kwamba hela ipotee mifukoni ni sifa kwa kilanja, lakini ukiangalia zimepotea kwa hao wanyonge wanaotetewa matajiri wamebaki na utajiri wao, tujiulize kati ya tajiri na mnyonge nani amepoteza, nani ameumia na nani anaelalamika?