MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Nimeisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri jana.
Nikiri sijawahi kumwona na kumsikia Rais Samia akiongea kwa namna ile.
Hotuba yake ilibeba ujumbe mzito ulioelekezwa kwenye anuani tatu, hivyo, hadhira tatu; wananchi wa kawaida, wanasiasa na Jumuiya ya Kimataifa.
Kwa andiko hili ningependa nijikite na anwani ya Wanasiasa na Wananchi.
Aidha, Rais Samia pia ni mahiri wa kufikisha ujumbe kwa njia ya fasihi. Kwenye fasihi kuna mawili yaliyojichomoza; samaki na muhali. Hilo la muhali pia nitalizungumzia kwenye andiko litakalofuata.
Ndio, na mashambulizi ya Samia kwenye anwani ya pili; wanasiasa, wala hakuyachelewesha.
“ Ukimya wangu si ujinga. Anayenyamaza kimya sio mjinga, na kupiga kelele si werevu.” Alitamka Rais Samia.
Kwamba kuna wanasiasa wameshasahu mapito waliyopitia. Si zamani sana. Kwamba hizo R4 wamezigeuza kuwa kichaka cha kufanya yasio ya taratibu.
Na sasa?
Rais wa Jamhuri ana taarifa nyingi.
Na hapa Rais Samia anazo taarifa na anawashukia wanasiasa hao kama mwewe;
“ Kumepangwa kushusha moto mpaka Samia aseme basi nimesarenda, naondoka. Hiyo Serikali au Serikali ya samaki?!”
Anaacha swali kwa hadhira yake ya kwanza; Wananchi.
Si ndio, kwa kauli hiyo ya Samia, basi, kuna ujumbe ameupeleka, kwamba ‘ The Lady is not for quitting.’
Kwamba Mama si wa kuachia ngazi na kuondoka.
Yumkini hao wenye kufikiri hivyo, Samia anawaambia Wananchi, kuwa wanasiasa hao hawamjui Samia.
Swali:
Jamhuri ya Samaki ikoje?
Jibu:
Ilivyo bahari ina samaki wa kila aina. Kuna nyangumi, papa, chewa, pweza, changu, ngisi na wengi wengine, bila kuwasahau dagaa.
Kwenye Jamhuri ya Samaki hakuna mifumo wala taratibu. Kila samaki anajiamulia vyake. Chewa atamla pweza, changu atamla kibua ili mradi ni vurugu tu baharini.
Na kuna samaki mdogo anaitwa kitakange. Wavuvi wa maji chumvi wanamjua vema samaki huyu mdogo lakini mwenye vurugu nyingi. Kitakange anaweza hata kuambaa baharini ubavuni mwa nyangumi bila hofu ya kumezwa.
Kitakange huyu ana sifa pia ya kuwachuza wenzake kwa maana ya kuwaponza hata samaki wakubwa baharini. Ni hivi, mvuvi anapotega gema baharini, gema lile lina matundu madogo madogo.
Samaki huyu kitakange huwavuta samaki wenzake na hata wale wakubwa hata wakaingia gemani. Wakati kitakange anapenya kwenye tundu za gema, samaki wenzake hubaki gemani. Hapo mvuvi huwafungia kirahisi.
Ni bahati mbaya, hata kwenye nchi yetu, tuna viongozi na wanasiasa wachache wenye tabia za samaki kitakange.
Nini Tafsiri yake?
Kimsingi mengine wayafanyayo baadhi ya wanasiasa ni ya kuturudisha nyuma. Ni misingi mizuri aliyoiweka Rais Samia ya R4 ambapo Maridhiano ni ‘ R’ Mama wa zote nyingine.
Kwamba yote yanazungumzika ili kupelekea mageuzi, uhimilivu na ujenzi mpya wa nchi. Hatukuwa nayo hayo, mpaka juzi tu, tulikuwa na watu waliokimbia nchi.
Ni ukweli, kuwa kama nchi, matukio yanayoendelea ya utekaji na mauaji yametuletea fadhaa na aibu kubwa. Yanaharibu taswira ya nchi yetu. Nchi tuliyozaliwa na tunayoipenda.
Lakini, dawa yake haiwezi kuwa kulifuta jeshi letu la polisi. Sote tuna wajibu wa kushiriki ulinzi wa pamoja kwa kujihami tukishiriana na polisi. Ndio tafsiri halisi ya falsafa yetu ya ulinzi jumuishi ya zama kwa zama- Total Defence.
Ni Tafakuri Jadidi.
Maggid Mjengwa.
Dar es Salaam.