Niwapongeze pia na mimi Mods Invisible wote haswa wa jukwaa la siasa kwani kipindi cha kampeni halikuwa jukwaa lilikuwa uwanja wa vita kwa maneno ya kukashifiana na kejeli ila mods walielewa na kuwaachia watu uwanja... Ilikuwa ni kama kwenye mechi za watani wa jadi hapa bongo halafu refa anaamua kupeta rafu zote apigi kipenga wala hatui kadi nyie uaneni tu....
Ila naona hali ile ya kampeni inaendelea mpaka sasa kuna watu wanazoea yaani ukipishana nae kidogo anapoteza busara kabisa kwa matusi ya nguoni kabisa....
Uchaguzi ushapita turudishe nidhamu ile iliyokuwepo ya JF..... Kuna mahali nilisoma bwana mmoja yaelekea ni mzee aliandika kwa uchungu sana kuwa pamoja na faida alizozipata hapa JF kwa mwaka huu ila ametukanwa mno na watu anaooamini ni vijana wadogo mno na labda hata ni watoto wake....