Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 33
- 104
Kibu Denis ndio kiungo mshambuliaji pekee aliyebaki kuokoa jahazi la Simba, mechi ya leo angeimaliza mapema kabisa.
Kwa sasa tutake tusitake mchezaji Kibu Dennis ana umuhimu mkubwa sana ndani ya timu yetu, bila yeye Simba haionekani kabisa kucheza dimbani.
Tukubali tusikubali Kibu Dennis ambaye nasikia yuko Marekani kwa mambo ya kifamilia (Kama kweli lakini maana viongozi wetu hawaaaminiki) anaweza kufanya mambo ambayo huwezi kuamini kama alivyowaharibu wale waarabu siku ile.
Kwa uchezaji wa JKT, Kibu angeweza kabisa kushirikiana na akina Mpanzu kuiangamiza kabisa Kagera Sugar.
Japokuwa Kibu hakucheza kule Bukoba na Simba ilishinda kwa idadi kubwa ya mabao lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa kukosekana kwa mchezaji huyu kunaiweka simba katika wakati mgumu sana.
Leo timu yetu imecheza utadhani timu ya mtaani, haina kabisa mbinu za kiufundi za kuwazidi wale JKT, ikiwa katika hali hiyo Kibu angeweza kupasua mabeki wale kwa nguvu na chenga zake na kuwachosha sana mabeki wa JKT, kumkosa KIbu uwanjani kwa sasa ni hasara sana.
Kukosekana kwake pia kumesababisha kocha awe anajiingizia tu wachezaji bila mpango, mara Mashaka, mara Zimbwe, mara Mutale, mara Mukwala, hakuna kabisa mipango na mbinu, hivyo njia pekee wakati mwingine mipango ya kocha ikiwa mibovu ni kuwategemea wachezaji aina ya Kibu kufanya maamuzi magumu.
Naipa asilimia ndogo sana Simba kutwaa ubingwa msimu huu kwa sababu hawachezi soka ukawa na uhakika kuwa mechi ijayo watacheza vile vile.Na ikikwama mechi moja tu wamekwisha, kuna timu ngumu sana kwenye ligi ya msimu huu, raundi ya 2 tunaenda kwao Namungo, Fountain Gate, Tabora, Coastal, Ken Gold, bado hujacheza na Yanga, Azam, Singida, hizo mechi ni ngumu sana na kwa timu ilivyo yenye viungo wakabaji kuliko wachezeshaji, napata hofu kubwa kuwa tunaelekea kubaya huko tuendako.Time will tell.
Soma Pia: FT: Simba SC 1 - 0 JKT Tanzania | NBC PL | KMC Complex | 24.12.2024
Ushauri wangu:
1. Uongozi ukae na kocha na kumweleza kuhusu kiwango cha timu kutoridhisha
2.Kuongeza wachezaji dirisha dogo hasa eneo la beki wa kati, kiungo mchezeshaji na mshambuliaji
3.Kamati ya ufundi iwe makini sana katika kila mechi kwani uwanja wa KMC tayari umeshaharibiwa na wale wahuni wa Jangwani
4.Mkakati uwekwe mechi ya mwisho vs Singida Black Stars, hii ni mechi ngumu mno kwetu na kwa aina ya wachezaji wetu ukilinganisha na wale Singida, kazi ipo siku hiyo.
5.Nawasihi sana viongozi na wanachama kushikamana katika dakika hizi za mwisho