Tafadhali nawaomba wanajf muokoe jahazi hili

Torabola

Member
Dec 8, 2020
51
69
#1
Wakuu nawasalimu kwa heshima zote..
Mimi ni muhangaikaji mwezenu, niko katika harakati za kutafuta riziki ili mkono uende kinywani...
Kama tujuavyo vijana wengi tupo ktk zahama kubwa ya ukosefu wa ajira hapa nchini haswahaswa graduate wa kada mbalimbali, hivyo basi inabid kama kijana ili maisha yaendelee haina haja ya kuchagua kazi kwan mambo yamekua tight mno..
Kufupisha story nikwamba nimeamua kuingia ktk kampuni ya ulinz inayoitwa GARDAworld zamani ikijulikna km kk security..
Nimefuzu kwa hatua ya awali ambapo vipimo pamoja na ukaguzi wa vyeti vyote hkn shida, ila tatzo nimekosa wazamini wawili ambao wanatakiwa wawe watumish wa serikali, au wa kampuni binafsi lkn wawe na vitambulisho vya kazi.Kusema ukweli sina ndugu ambae amekidhi hivyo vigezo na ukizingatia mimi ndo nilibahatika angalau kufuta ujinga ktk familia hivyo nimeshindwa kuwapata.Mwisho wa kupeleka wazamini ni jumanne, chondechonde ndugu zangu naombeni msaada wenu hakika hali ni mbaya mtaani, inafikia hatua unaomba kibarua cha kufanya usafi unaambiwa nafas hakna .
Ombi langu kwenu, kwa yoyote anayeweza kunisaidia juu ya Hilo naomba anisaidie jmn mana nimetingwa. Tusaidiane angali tupo hai,
Natanguliza shukrani,
Namba zangu +255673438548.
adamngalawa84@gmail.com.
 
Aise labda urudi kwenye taasisi za elimu ulizosomea kama primary na secondary mpaka chuo ukawaombe hao maana ni imani yangu wanafikika kwa urahisi kuliko huku mitandaoni, pamoja na yote kila la kheri mkuu nakuombea upate hitaji la moyo wako.
 
pole sana nahisi ni kwa kiasi gani kutokuwa na kipato na shughuli ya kufanya kunavyoumiza.
samahani ndugu kwa nitachoandika lakini uhenda kikawa msaada kwako au kwa wengine.
ningekuwa mimi ni bora niuze karanga au mishkaki kuliko kuwa mlinzi hasa ukizingatia ni kijana na nguvu zangu.(na nimewahi fanya hivyo mtaji nilipata kupitia kubebe zege).
kwanini nibora kufanya hizo biashara kuliko kuwa mlinzi:
1. kipato utachokipata kwa biashara hakiitaachana sana na mshahara wa ulinzi.
2. unapata fursa ya kujifunza biashara namna ya kumanage mambo, pesa na muda wako.
3. mtaji ukikuwa unaweza kukuza biashara yako kwa level za juu zaidi.
4. utakuwa na afya nzuri, walinzi wengi wanazeeka kabla ya wakati kwa sababu hawapati muda wa kutosha wa kupumzika wengi wanakesha na mchana wanaforce kufanya shughuli zingine mwisho wake ufanisi unakuwa zero.
5. kuwa jamii kukutazama kwa mtazamo mzuri, tofauti na walinzi wengi wanaonekana njaa na wakuda kutokana na baadhi yao wanaoichafua kazi hii kuwa na tabia za ajabu ajabu hasa wanapokuwa mawatchmen kwenye ofisi fulani.
6. kukua kiakiri kwani kupitia changamoto za biashara akili yako itakuwa inawaza ni kwa namna gani ya kutatua changaoto hizo ili ufanikiwe zaidi lakini ukiwa mlinzi unaweza ukabweteka kwa sababu ya uhakika wa mshahara.


kujiajiri ni kugumu lakini kunawezakana kwa kila mtu anayeamua na kukubali kuvumilia msoto wa muda fulani, kwabahati nzuri hata huo msoto ni sehemu ya kufanya ufanikiwe zaidi.
unaweza ukaona kazi hiyo ni msaada kwa sasa na kukwepa kazi ambazo zitakufanya uingie kwenye msoto lakini baadae utakujajuta.
kazi ya ulinzi waachie wazee na wastafu.
 
Tatizo mkidhaminiwa mwishowe mnatutia katika matatzo yasiyotuhusu

Unapewa kazi sijui lindo unashawishiwa watu wanaiba mwishowe unatokomea wadhamini wanapata shida ...

Kazi za ulinzi ukiamua kuzifanya kama ulivoamua kufanya kwa kuwa umekosa cha kufanya risk ni kubwa sana
 
Mimi sitarudia kudhamini mtu aisee! Nilidhamini mtu akaenda kushusha injini ya Scania, bahati nzuri tulimkamata kabla hajavuka mpaka wa Kenya!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom