TADB kwa masharti haya bakini tu na hela zenu, tutaenda kukopa benki za kibiashara

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,290
7,860
Tar 12/10/2018 mmoja kati ya viongozi wa benki ya maendeleo ya kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank) alikuja kuongea na wanachama cha ushirika Madibira. Ushirika unawanachama 3147 ambao kila mmoja anamiliki eneo la hekta moja (2.5 ekari). Katika maelezo yake ya kuipamba benki hiyo alisema kuwa benki hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia wakulima nchini kote. Aliongeza kuwa benki hiyo hutoza riba ya 8% - 12% ya pesa. Lakini masharti yao ni yafuatayo.

1: Mkopeshwaji toka benki ni chama.

Hapa alieleza kuwa wao watakopesha chama na chama kitamkopesha mkulima. Kwamaana kuwa wao hawahusiki na mwanachama gani kakopa kiasi gani!. Hapa chama cha ushirika kinabeba dhamana ya kuwa mkopeshaji wa pili na mkopaji wa kwanza toka benki. Chama kinachukua majukumu ya udhamini na ukopeshaji.

2. Masharti kwa chama cha ushirika

Chama cha ushirika kinatakiwa, kuandika barua ya maombi na kuituma makao makuu ya benki, kuitisha mkutano maalum na kuwaambia wanachama lengo la kujiunga na kuwatumia muhtasari, kupeleka nakala ya kitabu cha wanachama, katiba ya chama, TIN ya chama, bank statement za chama, taarifa za madeni ya chama, taarifa za kibiashara za chama, taarifa ya mkaguzi wa vyama vya ushirika, leseni ya usajili wa chama na ratiba ya zao (kukatua, kuwatika mbegu, kuvuruga,kupanda,uwekaji mbolea,magugu mpaka uvunaji) na Mali za chama kutumika kuchukulia mkopo.

Kwakifupi kuhusu Mali za chama ni ardhi, majengo, miundo mbinu ya maji na barabara, magari, trekta, kombain, rice milling machine, ofisi mbalimbali .

3: chama kitakopesha pembejeo za kilimo kulingana na kalenda ya zao.
Hapa alifafanua kuwa watatoa mbole, dawa za magugu na pesa zinazohitajika kwa wakati husika tu.

Hayo ni baadhi ya masharti ya benki hiyo. Kutokana na hayo naomba niwaambie kuwa bakini tu na hela zenu. Benki nyingine washindani kama CRDB, NMB na MUCOBA wanatoa pesa kwa wakulima moja kwa moja, chama huthibitisha tu kuwa muombaji ni mwanachama au la!. Pia taarifa mnazozitaka ni very confidential na ni sawa na kukikabidhi chama na huenda mwisho wa siku yakatukuta ya kapunga kuuzwa kwa wawekezaji.

Tulishawahi kupata mikopo ya matrekta na Powertila toka taasisi mbalimbali ikiwemo na suma JKT lakini chama hakijawahi kuweka poni Mali zake, mikopo huwa ni kati ya mwanachama na mkopeshaji. Lakini kwa masharti yenu haya,
Bakini tu na hela zenu ni bora tukakope kwenye benki za 20% - 30% ambazo hazirisk Mali za chama chetu kuliko kimkopo chenu chenye masharti kibao utafikiri tunataka kuchumbia.
 
Kiongozi,

Naomba nikufahamishe kuwa TADB ikiwa kama Taasisi ya Maendeleo ya Fedha (DFI), TADB inajitofautisha na mabenki mengine katika mambo makuu yafuatayo:

Mafunzo: TADB hutoa mafunzo kwa wakulima wadogo wadogo ili kuwajengea uwezo katika usimamizi wa fedha, utawala bora wa vikundi na vyama, utunzaji wa kumbukumbu na utengenezaji wa miradi inayokidhi masharti ya mikopo kutoka katika mabenki na taasisi za fedha.

Riba na Masharti: TADB inatoa mikopo kwa riba nafuu (chini ya riba ya soko) na kwa masharti yanayozingatia hali halisi ya kilimo cha mazao husika.

Marejesho: Marejesho ya mkopo hufanywa baada ya mavuno na hivyo vipindi vya marejesho hutofautiana kutegemeana na jinsi misimu ya uvunaji wa mazao husika ulivyo.

Dhamana: Hati za kimila za mashamba, dhamana za taasisi washirika kama vile PASS na Benki Kuu, dhamana nyingine ikiwemo mazao yaliyohifadhiwa kwenye maghala.

Usimamizi wa Fedha: TADB inafanya usimamizi wa fedha za maendeleo ya kilimo ikiwa ni pamoja na usimamizi wa Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogowadogo (Smallholder Credit Guarantee Scheme) unaolenga kuchagiza benki na taasisi za fedha kuongeza ukopeshaji katika sekta ya kilimo, na Mfuko wa Kuwezesha Ubunifu Vijijini (Rural Innovation Fund).

Wateja wa TADB: Wakulima wadogowadogo, wakulima wa kati na wakubwa; benki za maendeleo ya jamii, vyama vya kuweka na kukopa, taasisi ndogo za fedha, vyama vya ushirika na taasisi au vyama vya wakulima na wanunuzi na wachakataji wa mazao ya kilimo.

Hivyo, masharti yaliyowekwa yamezingatia hali halisi ya sekta ya kilimo lengo likiwa ni kuwapata wakulima wenye nia ya dhati ya kufanya kilimo biashara na si kukopa fedha kwa malengo kinzani.

Naomba nikutajie baadhi ya vyama vilivyokopa na kufanya vizuri katika kuhudumia mikopo yao. Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Ushirika wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo Korogwe, Vyama vya Ushirika vya Ngara, Karagwe na Kagera kwa uchache tu.

Nakuomba, utumie fursa ya uwepo wa Benki ya Kilimo katika kuchagiza shughuli zenu za uzalishaji.

Zaidi, naomba nikujulishe kuwa katika kuhakikisha Benki inawafikia wakulima wadogo nchi nzima, TADB imeanzisha Mfuko wa Dhamana kwa Mikopo ya Wakulima Wadogo Wadogo hujulikanao kama Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo Wadogo (SCGS) ambao unadhamini mikopo kwa wakulima wadogo wadogo hadi kufikia 50% ya mkopo unaotolewa na benki za biashara.

Kwa sasa, mabenki ambayo yameingia makubaliano na TADB katika kutoa huduma hii ni NMB, CRDB na Benki ya Posta ambazo zinategemewa/zinatoa kuanza kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo.

Hivyo, naomba ufike kwenye moja ya matawi hayo ili uweze kukopeshwa kupitia SCGS.
 
Mkuu naweza kukuchek inbox kwa msaada kidogo. Nimependa maelezo yako kwa kina, ila ninamaswali machache ningependa kukuuliza.
 
Hapo utakuwa unasubiri embe chini ya mnazi labda aje kwa ID nyingine
IMG_20200823_203454_146.jpg
 
Back
Top Bottom