Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,410
- 3,646
Watu wasiojulikana wamevamia na kuchoma moto Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Silambo iliyopo Kijiji cha Nsungwa Wilayani Kaliua Mkoani Tabora na kuteketeza baadhi ya nyaraka na samani zilizokuwepo ndani ya ofisi hiyo.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo Mashaka Mpuya tukio hilo la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa ofisi hiyo ya Mtendaji wa Kata limetokea majira ya usiku kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wananchi kwenye kata hiyo wamekua hawamtaki Mtendaji wao wa Kata Kijijini hapo.
Kufuatia tukio hilo kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya Kaliua imefika kushuhudia madhara yaliyotokea ambapo mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Gerald Mongella amesema kilichofanyika ni uvunjifu wa amani hivyo Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hilo ambapo ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka popote pale walipo wale wote waliofanya tukio hilo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.