Tabora: Wakamatwa wakiwa na Magamba 172 na kucha 16 za Kakakuona

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,817
Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao amesema watuhumiwa wawili walikutwa na Nyara hizo ikiwemo Ulimi na Maini ya mnyama huyo pamoja na Magamba ya Kiboko.

Pia, watu 38 wamekamatwa kwa kujihusisha na matukio ya wizi wa Pikipiki 10, uvunjaji na wizi wa Mifugo ambapo Ng’ombe 24 walioibwa maeneo mbalimbali wamepatikana.

Aidha, Kamanda Abwao amesema wanawashikilia watu 21 wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji kwa kutumia mapanga na watafikishwa Mahakama baada ya Upelelezi.

=====================

Watu 61 wamekamatwa na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Tabora katika matukio mbalimbali.

Katika tukio la kwanza, watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni magamba 172, ulimi, maini pamoja na kucha 16 za mnyama aina ya kakakuona na magamba matatu yanayodhaniwa ya mnyama kiboko.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema leo Jumatano Novemba 23, 2022 kuwa mbwa maalum wa unusaji walifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wilayani Kaliua.

Katika tukio lingine, watu 38 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha katika matukio ya wizi wa pikipiki, uvunjaji na wizi wa mifugo ambapo pikipiki 10 na ng’ombe 24 zilizoibiwa maeneo mbalimbali kupatikana.

Kamanda Abwao amesema uchunguzi wa awali umebaini pikipiki hizo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu na kwamba wamefanikiwa kukamata mali mbalimbali kama runinga 13, redio aina ya subwoofer tano, kichwa kimoja cha cherehani, pasi za umeme 2, mashine ya kukatia mbao 1 na toroli 1.

Kuhusu watuhumiwa wa mauaji, Kamanda Abwao amesema wamekamatwa watuhumiwa 21 wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji kwa kutumia mapanga.

"Watuhumiwa wanatuhumiwa kuhusika katika matukio ya mauaji na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika"Amesema.

Kamanda Abwao amewataka wazazi kuchunguza nyendo za watoto wao ili wasijihusishe na uhalifu kwani katika watuhumiwa 38 wa wizi, wapo watoto walio na umri chini ya miaka 18.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom