LGE2024 Tabora: Ulevi, Matusi na Kujitenga ndio sababu Wananchi kumpigia Kura ya 'Hapana' Mgombea Uenyekiti

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,107
2,647
Wananchi wa kitongoji cha NKENE,kijiji cha MAGULYATI,kata ya LOYA wilaya ya UYUI mkoani TABORA wamesema sababu za kumpigia kura za Hapana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa kitongoji chao NYOROBI NANGI ni kutokuwa na ushirikiano na wananchi pamoja na tabia za ulevi na matusi.

Wakizungumza na CG FM kwa njia ya simu,baadhi ya wananchi wa kitongoji cha NKENE wamesema aliyekuwa mgombea kiti hicho hana ushirikiano na wananchi wake kwa sababu hairuhisiwi kufika nyumbani kwake bila sababu na amekuwa akitumia kilevi muda mwingi na kukosa muda wa kusuluhisha matatizo yao.

Jumanne ya Tarehe 2 Desemba,2024 Msimamizi wa Uchaguzi mkoa wa Tabora Elihuruma Nyela Aliiambia Cg Digital kuwa Vitongoji vitatu vya Halmashauri ya Uyui vitafanya uchaguzi kwa mara ya pili.

Vitongoji hivyo ni Kitongoji cha Stesheni Kata ya Lolanguru mgombea alifariki, Kitongoji cha Mchanganyiko kijiji cha Ipululu Kata ya Igalula mgombea alifariki na Kitongoji cha Nkene kijiji cha Magulyati Kata ya Loya mgombea alipigiwa kura za hapana.

Nyela ameeleza kuwa uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku arobaini (40) tangu uchaguzi kufanyika.
 
Back
Top Bottom