Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 28,951
- 30,250
Kada wa Chama cha Mapinduzi aliyefahamika kwa jina la Justine Kiatu, anadaiwa kujiua baada ya mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rajabu Lupanda kutangazwa mshindi wa nafasi ya uwenyekiti wa Kitongoji cha Ikomwa Mlimani mkoani Tabora, akimshinda Edward Petro wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkuu wa mkoa huo, Paul Chacha ameeleza kuwa marehemu Kiatu alijiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu aina ya Ruruka mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumzi kifo hicho kwenye mkutano wa wakulima, Chacha ametoa wito kwa wananchi kuwa na uvumilivu wa kisiasa hususani nyakati za uchaguzi.