Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 304
- 641
Mambo yanayo zuia mafanikio kwenye maisha Tanzania ni mengi sana na ukiwachunguza sana watu waliofanikiwa utagundua kuwa kuna tabia au mambo kadhaa yanayoshabihiana kati yao.
Pia ukiwachunguza watu walioshindwa au ambao hawajafanikiwa, utabaini pia kuna tabia au mambo kadhaa yanayofanana kati yao.
Hawana vipaumbele wala muda wa kuweka malengo na vipaumbele kwenye maisha yao; wao huishi tu kulingana na lile linalokuja mbele yao.
Watu waliofanikiwa nao wanakosea, lakini hujifunza kutokana na makosa yao na siyo kutengeneza visingizio.
Kukusaidia kuweka na kutimiza malengo yako.
Ni muhimu kujifunza kuweka kwenye matendo mawazo na mipango yetu mbalimbali kuliko kuizungumzia pekee.
Watu ambao hawatafanikiwa huahirisha kila jambo, huamini kuwa maisha yao yanajengwa kesho na si leo. Hili ni tofauti kwa watu waliofanikiwa kwani wao huamini kuwa maisha ya kesho huandaliwa leo.
Jibu la hapana humtenga mtu na mipango, watu, na hata vitu visivyokuwa na umuhimu kwenye maisha na malengo ya mtu husika.
Hivyo watu wasioweza kusema hapana, kamwe hawawezi kufanikiwa kwani huchukuliwa na kila mawimbi kisha hushindwa kufanikiwa.
Watu waliofanikiwa hujifunza mambo mengi kadri wawezavyo ili kuongeza maarifa na uelewa wao. Maarifa sahihi na ya kiwango cha kutosha, yatakuwezesha kufanya maamuzi sahihi na bora kwenye maisha yako.
Ikiwa husomi vitabu, makala (mfano hii), kusikiliza na kutazama vipindi vinavyoongeza kiwango chako cha maarifa; kamwe huwezi kufanikiwa.
Ni muhimu kama mtu anapenda kufanikiwa akajifunza matumizi mazuri ya pesa. Hii itamwezesha kutumia pesa kuendeleza na kufikia ndoto zake.
Pia ukiwachunguza watu walioshindwa au ambao hawajafanikiwa, utabaini pia kuna tabia au mambo kadhaa yanayofanana kati yao.
1. kutojali muda
Mafanikio yamefugwa kwenye muda. Ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima ajifunze kutumia muda wake vyema. Watu wasiofanikiwa hawana mipaka; huchelewa kila mahali, pia hawathamini muda wa wengine.Hawana vipaumbele wala muda wa kuweka malengo na vipaumbele kwenye maisha yao; wao huishi tu kulingana na lile linalokuja mbele yao.
2. punguza visingizio
Walioshindwa hutoa visingizio vikubwa; husingizia na kulaumu kila kitu. Kila mara watu hawa hutafuta njia ya kuficha udhaifu wao kwa njia ya visingizio.Watu waliofanikiwa nao wanakosea, lakini hujifunza kutokana na makosa yao na siyo kutengeneza visingizio.
3. malengo
Malengo ni ramani muhimu ya kukuongoza kufika kwenye mafanikio au kutimiza ndoto zako. Watu walioshindwa hawana malengo wala hawafahamu faida za kujiwekea malengo maishani mwao.4. mwenzi sahihi wa maisha
Swala la mwenzi sahihi wa maisha linapuuzwa na watu wengi bila kufahamu umuhimu wake. Mwenzi sahihi kwenye maisha atakuwezesha kufanya mambo mbalimbali kama vile:Kukusaidia kuweka na kutimiza malengo yako.
- Kukushauri na kukutia moyo.
- Kukusaidia katika mipango na mikakati ya kutimiza ndoto zako.
- Kujali na kuheshimu hisia na utu wako.
5. matendo
Watu wengi ni wazungumzaji kuliko watendaji. Hili ni kinyume kwa watu waliofanikiwa kwani wao huweka kwenye matendo zaidi bila hata kujali kama watakwama au laa.Ni muhimu kujifunza kuweka kwenye matendo mawazo na mipango yetu mbalimbali kuliko kuizungumzia pekee.
6 kuharisha sana
“Nitafanya kesho”, “Bado kuna muda”, “Ni mapema sana kufanya hili”, “Bado najifikiria”, n.k. Ni baadhi ya kauli zinazopendwa na watu wanaopenda kuahirisha mambo.Watu ambao hawatafanikiwa huahirisha kila jambo, huamini kuwa maisha yao yanajengwa kesho na si leo. Hili ni tofauti kwa watu waliofanikiwa kwani wao huamini kuwa maisha ya kesho huandaliwa leo.
7. kusema hapana
Kila mara nimekuwa nikisisitiza kuwa jibu la hapana lina nguvu na umuhimu sana. Kusema hapana ni jambo linalofanywa sana na watu waliofanikiwa kuliko wale wasiofanikiwa.Jibu la hapana humtenga mtu na mipango, watu, na hata vitu visivyokuwa na umuhimu kwenye maisha na malengo ya mtu husika.
Hivyo watu wasioweza kusema hapana, kamwe hawawezi kufanikiwa kwani huchukuliwa na kila mawimbi kisha hushindwa kufanikiwa.
8 kutopenda maarifa
Ni watu wachache sana ndiyo wanaofahamu umuhimu wa maarifa katika mchakato mzima wa kufanikiwa.Watu waliofanikiwa hujifunza mambo mengi kadri wawezavyo ili kuongeza maarifa na uelewa wao. Maarifa sahihi na ya kiwango cha kutosha, yatakuwezesha kufanya maamuzi sahihi na bora kwenye maisha yako.
Ikiwa husomi vitabu, makala (mfano hii), kusikiliza na kutazama vipindi vinavyoongeza kiwango chako cha maarifa; kamwe huwezi kufanikiwa.
9. matumizi mabaya ya pesa
Hili ni janga linalowakabili watu wengi ambao bado hawajafanikiwa. Watu wengi hupata pesa lakini zinakwisha bila kujua wamefanya nini chenye manufaa kwao.Ni muhimu kama mtu anapenda kufanikiwa akajifunza matumizi mazuri ya pesa. Hii itamwezesha kutumia pesa kuendeleza na kufikia ndoto zake.