Tabia yake ilimponza akaharibu meeting

De Opera

JF-Expert Member
May 23, 2013
761
1,602
Habari za muda huu wakuu? Ninaimani mnaendelea poa, lakini poleni kwa wale mnaokabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo 'Kiafya' na nina imani mtarejea katika utimamu.

Wakuu, katika kuhakikisha tunapashana na kupeana yale yanayoweza kutuongezea elimu na kutusogeza mbele, leo nashuka na uzi huu.

Niliwahi kufanya meeting na dada mmoja ili tu tuweze kujuana vizuri japo kwa machache vile mimi nilikuwa katika muda wa kutafuta mwenza.
Siku ya meeting katika hoteli fulani Jijini Mwanza, nilikutana na huyo dada ila meeting haikuenda sawa. Kiukweli sikupendezwa na vile alivyokuwa akifanya pale, coz toka tulipofika muda wote alikuwa akiongea na simu, tena za mashoga zake. Tukiongea maneno mawili matatu, tayari kashapiga simu. Nilighafilika sana.

Mimi sikutaka kuonekana nimekerekwa. Wakati akiongea na simu, nilifungua simu yangu nikatafuta jina la mtu wangu wa karibu kabisa. Nikamtumia sms nikimwambia afanye kunipigia kama simu ya dharura halafu aniambie nahitajika ofisini haraka.

Nilifanya hivo ili tu nipate kumkwepa yule dada. Kiukweli nilifanikiwa, rafiki yangu alinipigia na nikaweka Loud Speaker
🔊
ili yule dada asikie.

Baada ya hapo, niliinuka nikachua waleti yangu nikatoa 15k kisha nikampa yule dada kwa ajili ya nauli na muda wake nilioupoteza kumuita aje pale. Japo alipokuwa akitokea si mbali sana na tulipokuwa.

Yule dada niliona amebadilika ghafla kashikwa na huzuni, simu yake akaifunga na kuiweka kwenye mkoba wake kisha akanishika mkono wa kulia na kuniuliza ni lini tena tutakutana pale, nami nikamwambia 'Tuombe uzima' kisha nikamuacha, sikutaka kumsindikiza hadi kwenye usafiri coz nisingependa nijue atataka atumie usafiri gani.

Toka siku hiyo.. Siku ya kwanza nilituma meseji 10, siku ya pili meseji 5, siku ya tatu meseji 2, siku iliyofuata meseji 0 na hadi leo sijawahi mtafuta kabisa.
Toka hapo nikasema 'Tabia zetu za wazi ndio hufanya tusonge au tusisonge mbele'.

Kuna kitu inaitwa 'Perception'. The way unakutana na mtu mara ya kwanza unam-study, ndio 70% ya mambo/tabia yake ya muda wote.
Jamani, kuna tabia hatuna budi kuzi-balance.

Kauli yangu huwa ni moja. "Usiogope kupoteza wakati ukitafuta kitu sahihi".

Ahsanteni wakuu!
 
Back
Top Bottom