KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
 
Pesa unamchangia mwanao Bado unalia
Kwani ulimzaa na nani?
Kama unaona unaibiwa si mwanao aache shule ubaki na pesa yako

Hakuna elimu Bure, usidanganyike na siasa
Hata hao wanasiasa wanalipia yote hayo na watoto wao wapo private schools
Angalia na huyu anaongea kama amekatwa kichwa. Aise nchi hii ndiyo maana viongozi wanawadharau sana wananchi kwasababu ya watu kama nyinyi.

Sasa hapa unaona umetoa bonge la hoja yaani. Au wewe ndio mwalimu mwenyewe unayechangisha michango iliyopigwa marufuku ili tu ikupunguzie ugumu wa maisha?
 
Hakuna elimu rahisi hiyo 500 yako haiwezi kumfanya mwalimu awe bilionea toa mtoto afanye weekly test
Ratiba iliyowekwa na serikali ya masomo/vipindi ina maana walioiweka ni wapumbavu ila walimu ndiyo wenye akili siyo?

Aise kama kuna mtoto ameadhibiwa kwasababu hajatoa mchango sijui wa mtihani ama anabaguliwa natamani mzazi aje PM yangu niwanyooshe hao walimu napeleka mahakamani mwenyewe ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine.
 
hii inchi ina ujingaujinga mwingi kuna vimichango vya kipuuzi ambazo hizo hela zinapigwa na wajanja wachache

umaweza kuambia mtihani buku wakati kuprint page moja ni 50au 100

ukija mtaani huku kuna michango ya usafi uliinzi shirilkishi inakusanywa kiholela na watu wanalipa kama mazuzu
 
Angalia na huyu anaongea kama amekatwa kichwa. Aise nchi hii ndiyo maana viongozi wanawadharau sana wananchi kwasababu ya watu kama nyinyi.

Sasa hapa unaona umetoa bonge la hoja yaani. Au wewe ndio mwalimu mwenyewe unayechangisha michango iliyopigwa marufuku ili tu ikupunguzie ugumu wa maisha?
We unaonekana ulivo kichwani

Sasa mchango wa mtoto wako unalia Nini?

Hata Tanganyika school pale michango ipo ila hutasikia Ridhiwani analia mtandaoni

Kwaiyo tuache kujadili mambo ya maana tikusikilize wewe unayelilia sh 200 ya mitihani
 
Hela ya mtihani tu tena kwa kila wiki unalalamika? Unamkatia tamaa hata mtoto mwenyewe..yaani hapo utaanza kumuuliza kwa ukali kwanin pesa kila wiki?

Usijue kuwa na yeye ataanza kuona hyo mitahani haina maana kwake kwasababu wewe kama mzazi umeshaizarau tayri.

Tuache kulalamika...
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Hela ya mtihani tu tena kwa kila wiki unalalamika? Unamkatia tamaa hata mtoto mwenyewe..yaani hapo utaanza kumuuliza kwa ukali kwanin pesa kila wiki?

Usijue kuwa na yeye ataanza kuona hyo mitahani haina maana kwake kwasababu wewe kama mzazi umeshaizarau tayri.

Tuache kulalamika...
Hela ya mtihani tu tena kwa kila wiki unalalamika? Unamkatia tamaa hata mtoto mwenyewe..yaani hapo utaanza kumuuliza kwa ukali kwanin pesa kila wiki?

Usijue kuwa na yeye ataanza kuona hyo mitahani haina maana kwake kwasababu wewe kama mzazi umeshaizarau tayri.

Tuache kulalamika...
Acheni hiyo tabia,shule ya msingi Mizimbini,iliyo Kibada na shule ya msingi Kibada,wana tabia hiyo....kama hamtaki kutoa mitihani simuache? Kwani mmelazimishwa?
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Walimu kama hamuwezi kuishi mjini,hamieni Burundi.Shule za msingi Mizimbini na Kibada zilizo Kibada kigamboni,wana tabia hiyo.Na mkiendelea na tabia yenu,tutawaweka hadharani kwa waziri.
 
Walimu wa Mizimbini na Kibada,shule za msingi zilizo kata ya Kibada kigamboni,wana tabia hizo sana.Sasa msipoacha ,taarifa zenu tunafikisha kwa wahusika.
 
Pesa unamchangia mwanao Bado unalia
Kwani ulimzaa na nani?
Kama unaona unaibiwa si mwanao aache shule ubaki na pesa yako

Hakuna elimu Bure, usidanganyike na siasa
Hata hao wanasiasa wanalipia yote hayo na watoto wao wapo private schools
Ni bora serikali itoe tamko kwamba elimu shule za serikali tulipe ada kuliko kufanya utapeli..
Kulipa kila siku 200 za test na kila jmosi kulipa 1000 za mtihani sio utapeli?

Mtoa post ana hoja nzr asipuuzwe
 
Yani wewe na akili zako tunaamini Kuna elimu ya Bure,
Unataka hadi uambiwe na Serikali kuwa elimu ni gharama
 
Ndy serikali itoe tamko kama ni ada tulipe kuliko kufanya utapeli
Haya
Subiri tamko la serikali
Endelea kupuuza ubunifu wa walimu kuwapa watoto wako majaribio kila wiki waone hao walimu ndo maadui

Serikali itakuridhisha Kwa kupiga marufuku michango na majaribio, wakijua wazi watoto wao hawasomi hizo shule
 
  • Thanks
Reactions: K11
Mtoto wa maskini atabaki kuwa wa maskini tu huwezi kukuta mzazi anaemsomesha mwanae english medium akaja kulalamikia mitihani ya wiki ni sisi kajamba nani ndio tunalalamika.
English medium hawana gharama za mitihani kila wiki. Walishajumlisha kwenye fees na Ream la karatasi kila term.
 
Back
Top Bottom