Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,715
- 13,467
JamiiForums imeingia makubaliano ya ushirikiano na Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) ili kupaza sauti zaidi kuhusu masuala ya unyanyasaji wa Wanawake na Watoto.
Fuatilia tukio la uzinduzi wa ushirikiano huo hapa
Ndugu Wanahabari,
Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s Dignity Forum – CDF) ni shirika la hiari, lisilo la kiserikali, ambalo limesajiliwa mwaka 2006. Lengo kuu la Shirika la CDF ni kutekeleza programu na mipango mbalimbali yenye kukuza, kutetea na kuboresha haki na ustawi wa mtoto wa Kitanzania, hasa mtoto wa kike katika Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar Es Salaam, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma na Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara.
Jamii Forums ni asasi ya kiraia iliyosajiliwa mwaka 2019 inayotetea na kuhamasisha haki za kidijitali, utawala bora, demokrasia na uwajibikaji. Moja ya malengo yake ni kusaidia kupaza sauti za wananchi na asasi nyingine za kiraia mtandaoni ili kujenga jamii yenye uelewa wa mambo anuai.
Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) na Taasisi ya Jamii Forums ambao ni waratibu wa Mtandao mashuhuri wa kijamii wa (JamiiForums.com) wanazindua ushirikiano wa kikazi kwa lengo la kukuza uelewa wa haki na ustawi wa mtoto wa Kitanzania katika harakati za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto ikiwemo mimba za utotoni, ukeketaji, ndoa za utotoni, ubakaji na ulawiti, vipigo, matusi na udhalilishaji wa utu wa mtoto.
Ripoti ya Haki za Binadamu ya Mwaka 2019 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (2019) ilieleza zaidi ya matukio 42,824 ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa polisi kwa mwaka 2016 hadi 2019. Matukio hayo yalibainishwa kuwa ni ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono, utumikishwaji kazi kwa watoto, ubaguzi wa watoto wanaoishi na ulemavu, ongezeko la mimba na ndoa za utotoni.
Utafiti wa Demographia na Afya (TDHS) wa mwaka 2015/2016 unaonyesha asilimia 27 ya wasichana kati ya miaka 15 hadi 19 walipata ujauzito. Kwa mwaka 2003 hadi 2011, wanafunzi 55 elfu waliacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni, wengi wakiwa kati ya umri wa miaka 13 hadi 18. Kwa kipindi cha Januari 2018 hadi Desemba 2019, LHRC ilikusanya matukio zaidi ya 2543 ya mimba za utotoni. Lakini tunaamini matukio mengi zaidi hayajaripotiwa. Katika matukio haya ya mimba za utotoni walimu wa kiume wanaotumia madaraka yao vibaya kuwarubuni wanafunzi wa kike kufanya ngono na matokeo huwa ni mimba za utotoni, waendesha boda boda pia hutumia kigezo cha kuwapa ‘lift’ wanafunzi wa kike kwa sababu ya umbali kati ya shule na makazi ya wanafunzi hawa na kuishia kuwarubuni na kuwapatia ujauzito.
Zaidi ya asilimia 90 ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa polisi ni matukio ya ukatili wa kingono, yakiwemo matukio ya ubakaji na ulawiti. Matukio haya ya ukatili wa kingono yamekuwa yakitokea zaidi majumbani. Ripoti ya ukatili wa kingono iliyotolewa na Jeshi la Polisi mwaka 2016, inasema asilimia 49 ya ukatili wa kingono hutokea nyumbani na asilimia 23 hutokea mitaani na asilimia 15 hutokea shuleni. Hii inaonyesha dhahiri kuwa ukatili wa kingono hufanywa na watu wa karibu sana na watoto ikiwemo wazazi na walezi wa kiume, wajomba, kaka, walimu wa shuleni na walimu katika taasisi za kidini. Matukio zaidi ya 43,487 ya ukatili wa kingono yaliripotiwa kwa mwaka 2018 katika vituo vya polisi.
Oktoba 2019, Mahakama ya Rufaa Tanzania ilitoa hukumu ya kesi ya Mahakama Kuu ya mwaka 2016 juu ya ndoa za utotoni. Hukumu hiyo ilikuwa juu ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 ambavyo vimeruhusu msichana wa miaka 14 na 15 kuolewa kwa ridhaa ya mzazi au mahakama. Vifungu hivyo vinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo basi Mahakama ya Rufaa ilitangaza umri wa mdogo wa kuolewa ni miaka 18 na kulitaka Bunge kurekebisha sheria hiyo. Lakini hadi sasa hakuna marekebisho yaliyofanyika na Bunge.
Utafiti wa Demographia na Afya (TDHS) wa mwaka 2015/2016 unaonyesha wanawake 36 kati ya 100 wenye umri kati ya miaka 25 na 49 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Takwimu hizi ni sawa na msichana mmoja kati ya wasichana watatu huolewa chini ya mika 18. Ndoa za utotoni zimekuwa zikiwanyima haki ya elimu wasichana na kuwaweka hatarini kupitia ukatili wa kingono, kihisia, vipigo na kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Sababu za ndoa za utotoni ni pamoja na umaskini uliokithiri, ukosefu wa elimu bora, mila na desturi kandamizi na kuwepo kwa sheria kandamizi (sheria ya Ndoa ya 1971).
Nchini Tanzania, ukeketaji ni kosa la jinai katika sheria ya kujamiiana (SOSPA) ya mwaka 1998 (kifungu 169A), lakini bado baadhi ya jamii zimekuwa zikifanya ukeketaji wa watoto wa kike. Ukeketaji umepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwa mwaka 2016 kutokana na juhudi mbalimbali za Serikali, asasi za kiraia na wadau wengine wanaopinga ukeketaji. Utafiti wa Demographia na Afya (TDHS) wa mwaka 2015/2016 unaonyesha, mwanamke mmoja kati ya 10 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wamekeketwa, huku asilimia 35 ya wanawake hao walikeketwa kabla ya kufikisha miaka mwaka mmoja. Sababu za ukeketaji zimetajwa kuwa ni njia ya kutunza ubikira wa wasichana kwa ajili ya heshima ya familia, ni njia ya kuonyesha msichana amekuwa mwanamke kamili, pia mangariba wanajiingizia kipato kutokana na ukeketaji.
Kumekuwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Asasi za kiraia, vyombo vya habari, wadau wa kimaendeleo na wadau wengine wanaotetea haki na ustawi wa watoto katika kuhakikisha watoto wanalindwa na kupatiwa haki zao stahiki.
Tanzania ina mifumo ya kulinda haki na ustawi wa mtoto ambayo imekuwa ikisimamiwa na Serikali. Kumekuwa na Mahakama za watoto (Juvenile Courts) ambazo zimekuwa zikisikiliza mashauri ya watoto waliokinzana na sheria, uwepo wa madawati ya Polisi ya jinsia na watoto na vituo vya mkono kwa mkono (one stop centres) maeneo mengi nchini Tanzania ambayo yanafanya kazi za utetezi wa haki za watoto na kuhakikisha haki inatendekea. Uwepo wa sheria, mikataba na sera mbalimbali inayolinda haki na ustawi wa mtoto, Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, Mkataba wa Afrika kuhusu haki na ustawi wa mtoto, Mkataba wa kimataifa wa Haki za watoto, Sera ya Maendeleo ya watoto. Sheria hizi zote zinamlinda mtoto dhidi ya ukatili na kuhakikisha hakiz zake zinalindwa bila ubaguzi wa jinsia, utaifa n.k.
Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya kazi katika kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii, ikiwemo wazee wa kimila, viongozi wa kidini, wazazi na walezi, wanaume na wavulana katika kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili dhidi ywa watoto. Pia, kumekuwa na elimu ya afya ya uzazi na kujitambua kwa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari ili kupunguza mimba za utotoni, wanafunzi hawa wamekuwa wakipewa mafunzo juu ya namna ya kuripoti matukio ya ukatili kwa Serikali za mitaa (vijiji), kwenye madawati ya polisi ya jinsia na watoto au kwa kupiga namba 116 bila malipo.
Juhudi nyingi zimefanyika lakini bado matukio ya ukatili dhidi ya watoto yanaendelea kushamiri sehemu mbalimbali za nchi kwa sababu bado jamii zinaendelea kukumbatia mila na desturi kandamizi, kuwepo kwa mfumo dume na rushwa katika taasisi mbalimbali. Lakini bado tutaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha vitendo hivi vinatokomezwa.
Tukiwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambazo huanza rasmi tarehe 25 Novemba hadi 10 Desemba kila mwaka, Taasisi za CDF na Jamii Forums zitashirikiana katika kupinga aina zote za ukatili wa kijinsia hasa ukatili wa kingono.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) unaonesha kuwa asilimia 84.5 ya vitendo vya rushwa ya ngono hufanyika kwa wanawake ambapo asilimia 15.4 hufanywa kwa wanaume. Kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa Demographia na Afya (TDHS) za mwaka 2015/2016 unaonyesha asilimia 36 ya wanawake nchini Tanzania wameolewa kabla ya kufika umri wa miaka 18. Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2019 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ilibainisha asilimia 84 ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa na vyombo vya habari mwaka 2019 ni ya ukatili wa kingono.
Tafiti hizi zinadhihirisha hali ya ukatili wa kingono nchini Tanzania, ambapo CDF na Jamii Forums tunakemea vitendo hivi vinavyodhalilisha utu wa mtu na ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu.
Hivyo basi, katika mapambano haya dhidi ya ukatili wa kijinsia, CDF imeingia makubaliano na Mtandao wa JamiiForums ili kuweza kutoa elimu na kufikia watu wengi zaidi Tanzania. Mtandao wa Jamii Forums unaongoza kwa kusomwa ndani na nje ya Tanzania ukiwa na zaidi ya wasomaji takribani milioni 10 kila mwezi. Hivyo basi, CDF na Jami Forums wataweza kutoa elimu kwa jamii juu ya sheria na sera zinazomlinda mtoto wa Kitanzania, mila na tamaduni zinazomkandamiza mtoto, wajibu wa mtoto kwa jamii, wajibu wa wazazi na walezi kwa mtoto na wajibu wa jamii kwa mtoto. Pia, elimu itatolewa juu ya namna ya kuripoti kesi za ukatili katika vituo husika (mfano Dawati la Jinsia na Watoto, Vituo vya mkono kwa mkono) ili kuwezesha upatikanaji haki.
Kwa ushirikiano huu kati ya CDF na Jamii Forums, tutaweza kupaza sauti na kutoa elimu kwa Jamii na wahanga wa ukatili juu ya haki zao, namna ya kuripoti kesi hizi na kuendeleza juhudi zinazofanywa na Serikali, Asasi za Kiraia, Wadau wa Kimaendeleo, Vyombo vya habari na jamii kwa ujumla katika kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Imetolewa na;
Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) na Jamii Forums (JF).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZINDUZI WA USHIRIKIANO KATI YA JUKWAA LA UTU WA MTOTO (CDF) NA JAMII FORUMS

Novemba 2020