Taasisi ya MOI yaanzisha Teknolojia mpya mbadala wa dawa za maumivu sugu ya mgongo na kichwa bila upasuaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
Dk-MOI-4-ba23-5ca326116d7a.jpg

Kwa mara ya kwanza Afrika, teknolojia mpya ya mbadala wa dawa za maumivu, imeanza kutumia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Hadi Aprili 28, 2023 jumla ya wagonjwa 18 wamepata huduma hiyo, ili kuepuka maumivu ya mishipa ya fahamu, ambapo huduma hiyo itaendelea kutolewa zaidi kwani takribani watu 70 huhitaji kwa siku huku kwa mwezi wakiwa 1,500.
IMG-20230428-WA0150.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respisius Boniface amesema huduma hiyo inatolewa kupitia maabara ya kisasa ya upasuaji ubongo bila kufungua fuvu la kichwa, ambapo gharama yake ni Sh milioni moja ndani ya nchi na Sh milioni 20 nje ya nchi.

Amesema “Hii ni huduma ya kutibu maumivu ya muda mrefu utakuta mtu anakuwa na maumivu kila siku hayaishi na tumekuwa tukipata wagonjwa hao anakwambia anaumwa mgongo kila siku wakija tunawapa dawa za maumivu na kila siku anakuwa kwenye dawa, sasa kutumia dawa kila siku sio vizuri."
IMG-20230428-WA0144.jpg

IMG-20230428-WA0142.jpg

Dkt. Boniface amesema katika utoaji wa huduma hiyo mpya madaktari wa MOI wanashirikiana na madaktari kutoka India, ili kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani.

Amesisitiza kuwa utoaji wa huduma hiyo ni juhudi za serikali kuhakikisha huduma ambazo zinatolewa nje ya nchi zinatolewa na ndani ya nchi, ikiwa katika uelekeo wa kwenda katika utalii wa matibabu.
dawa-za-maumivu-new-fb8a1dfa8332.jpg

IMG-20230428-WA0148.jpg

“Ndio maana tumeanzisha hii leo unachomwa kama sindano kwa kutumia mitambo tuliyonayo katika maabara ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu ku X-Ray za hali ya juu ambayo inamuelekeza daktari wapi pa kuweka dawa na kuchomwa kupitia mtambo,” amesema.

Amesema baada ya mgonjwa kupata huduma hiyo hatapata maumivu na ataruhusiwa kutoka hospitali siku ya pili au tatu.
IMG-20230428-WA0139.jpg
 
Back
Top Bottom