Taasisi ya manjano foundation kuendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Dodoma

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa LAPF House Mkoani Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani.


Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa LAPF House Mkoani Dodoma.

Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa

Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.

Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 712 646 322 au +255 718 010 107
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…