Kuelekea 2025 Taarifa za kuwepo kwa uchakachuaji matokeo zinaweza kuwa na lengo la kuwakatisha tamaa waliopanga kupiga kura kwa upinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,330
4,692
Kila kitu kichachofanywa na wanasiasa mara nyingi huwa kinakuwa na sababu nyuma yake, tayari kinakuwa kishapigiwa hesabu kuona nini faida yake na hasara yake.

Kauli au taarifa za kuwepo kwa uchakachuzi wa matokeo ya uchaguzi, au wizi wa kura huemda ni moja ya mbinu ya kupunguza idadi ya wapiga kura wa mrengo wa kushoto( wapinzani) kwa kuwa wao ndio wanakuwa waathirika wa moja kwa moja wa taarifa hizo hivyo kukata tamaa kushiriki zoezi zima la kupiga kura kwa kuona kura yao haina thamani kwani haiwezi kubadili chochote.

Huwenda hiyo ndio lengo la taarifa hiyo, kumbuka wa upande wao hawawezi kuacha kupiga kura kwa kuwa wanajua wao kura zao zitahesabika kuwa sahihi hivyo watajitokeza kwa uwingi wao kupiga kura.

Iwapo idadi ya wapinzani walikuwa wengi kuliko wale wa chama ambacho kimetangaza kuchakachua matokeo na wapiga wa upinzani wakakata tamaa kushiriki kipiga kura moja kwa moja watakuwa wamewapa ushindi wa kishindo wale wa chama kile kwani wao watakwenda kupiga huku hawa wakibaki kususia kumbe wangeshiriki zoezi kwa wingi wao wangeweza badili jambo.

Wanasema mchawi mpe mtoto akulelee, huwezi chakachua kura milioni moja kama wewe una moja, watu wasikate tamaa kupiga kura kwa vyama vyote, kwa raia wote kila mmoja aende kupiga kura kwa idadi kubwa ambayo haijawahi tokea ndio silaha pekee uliyonayo mwananchi.

Pia soma:Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
 
Back
Top Bottom