Taarifa za awali: Moyo wa Hayati Ndesamburo ulikuwa na matatizo makubwa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Wakati uchunguzi wa kifo cha Hayati Philemon Ndesamburo ukiendelea,taarifa za awali zinadokeza kuwa moyo wake ulikuwa na matatizo makubwa.

Kiongozi wa wachunguzi wa kitabibu,Prof. Elisante Masenga amesema kuwa taarifa hiyo ni ya awali na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye baada ya uchunguzi kukamilika.

R. I. P. Hayati Ndesamburo!

Chanzo: ITV Habari
 
Mara nyingi watu huwa hatusomi mambo mpaka mwisho.

Tunasoma sentensi mbili tatu za mwanzo, basi!

Chanzo ni ITV lakini mshikaji hajaona
Kama chanzo ni ITV hilo haliondoi ukweli kwamba mtu kasambaza habari za ugonjwa wa mtu aliyefariki.

Swali langu la msingi halijajibiwa.
 
RIP Mzee Ndesa
Wewe ni mfano wa kuigwa na kizazi cha Leo kwa jinsi ulivyopigana na maisha kiuchumi.
 
Swali lako umelielekeza kwa mleta mada kana kwamba ni yeye ndiye anazungumzia habari za mgonjwa wakati yeye kaleta habari zilizoripotiwa na ITV....

Kwa hiyo swali lako liko misplaced....
Hapa JF yeye ndiye kaleta habari. Swali halijawa misplaced.

Kwa sababu ITV wanaweza kuwa wamekosea na yeye akaendeleza makosa.
 
Hapa JF yeye ndiye kaleta habari. Swali halijawa misplaced.

Kwa sababu ITV wanaweza kuwa wamekosea na yeye akaendeleza makosa.

Sawa, hapa JF kaileta yeye.

Lakini pia kaweka chanzo cha alipoitoa.

Halafu wewe unakuja kumwuliza kama ana ruhusa ya kuongelea ugonjwa wake!

Yeye binafsi kama ndo angekuwa chanzo basi swali lako kwake lingekuwa halali.

Sasa habari iliyorushwa na kituo cha habari kinachoweza kuangaliwa na yeyote yule mwenye tivii wewe unamwuliza yeye aliyeileta hiyo habari ya ITV hapa kama ana ruhusa ya kuongelea ugonjwa wa marehemu?

Swali lako kwake liko misplaced, period, end of sentence.

Labda kama ungelielekeza kwao ITV ungekuwa sawa. Hapo kwa Petro si sawa.

Walau ungekuwa sawa endapo asingeweka chanzo cha alipoitoa hiyo taarifa.

Waulize ITV kama wana ruhusa ya kuongelea hizo taarifa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…