Taarifa ya haraka kwa RTOs Kigoma na Tabora

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Leo tarehe 12/4/2017 muda huu saa tano na dk 50.
Gari la NBS kutoka Tabora kwenda Kigoma. Basi hili limejaza kupita kiasi na abiria hawasikilizwi.
Kwa sasa gari ndio limetoka Kaliua kuelekea Usinge. Abriria waliosimama ni zaidi ya waliokaa.
Askari wa barabarani hawajachukua hatua yoyote.
Jamani tusisubiri kutangaziwa ajari na wakati tunaweza kuzuia.
Asante.
Taarifa hii nimeituma kwa RTO Kigoma na Tabora
 
Angalau ungeweka na namba za gari husika ili taarifa yako ichukuliwe kwa uzito mkuu. Thanks
 
Inaelekea ulikuwa na haraka sana wakati wa kuandaa hii taarifa
 
mkuu kama ishu gari kujaza sana abiria mbona daladala zinajaza hatusikii ajali labda kama utasema kuhusu mwendokasi wa basi
 
Hakuna mtu selfish kama Abiria. Wako makundi mawili
1. Abiria aliyekaa huwa hampendi alosimama, anaona anahaki zaidi kwasababu tu kabahatika kupata seat.
2. Waliosimama na Waliokaa hawapendi aongezeke abiria mwingine. Wanahisi baada ya wao kupanda tu hatakiwi mwingine aingie.

Huu ni utafiti 100% uko sahihi. Chunguza utagundua.

Reference, bandiko hilo hapo juu. Na wewe mwenyewe usiyependa abiria wenzako.
 
Nimecheka sanaa hahahahahahahahahahah....
 
Hunyu, angalau mara moja kwa mwaka binadamu anapaswa kutumia akili yake ili isioze.

1. Yule MMILIKI/MHUDUMU wa basi hakuwajaza abiria kwa kiwango hicho kwa kuwa anawapenda, ni kwa kuwa anataka hela zao.
2. Basi kujaza abiria kupita kiasi ni hatari kwa abiria wenyewe
(i) Suffocation, magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya hewa
(ii) Ajali, udhibiti wa chombo ni mgumu kinapozidiwa uzito na bila shaka unafahamu matumizi ya seat belts
3. Abiria akiyekata tiketi yake akaketi, hakutaraji usumbufu wa mtu mwingine kumuegemea begani au kusimama mbele yake
4. NI KINYUME NA SHERIA za nchi yetu kupakia abiria zaidi ya pendekezo la muundaji wa chombo husika.
 
Dereva mzuri ni yule asiyewasikiliza abiria... Wacha abiriwa wapige kelele lakini am sure dereva atawafikisha salama Kigoma...
 
0758 000 555 tuma ujumbe wako kwa namba hiyo uone hata dakika 10 haziishi
 
Asanteni sana kwa waliosoma uzi wakashauri na wengine kubeza.

Shukuraani za pekee kwa polisi wa daraja la Kikwete/Malagarasi wamelikamata gari na sasa dereva na konda wote wapo mikono salama.

Nitawajuza kitakachotokea. Kwa kadri nitakavyopata majibu kutoka kwa iformer wangu. Mm sipo kwenye gari lkn kuna raia mwema kaniaomba msaada.
 
Wameandikiwa charge sheet, gari limeruhusiwa kuondoka maana kuna mwanamke alikuwa anahtaka kujifungua. Dereva kaambiwa apeleke abiria hlf basi liende kituoni.
 
Wameandikiwa charge sheet, gari limeruhusiwa kuondoka maana kuna mwanamke alikuwa anahtaka kujifungua. Dereva kaambiwa apeleke abiria hlf basi liende kituoni.
sasa ndio mnaendelea na safari na abiria tuti kisa mja mzito? kwanini hao matrafik wasiite ambulance imbebe huyo mja mzito? kutoka hapo darajani hadi kigoma ni zaidi ya km 200 atafika salama kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…