Taarifa ya Balozi Dkt. Slaa kuhusu Mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,805
13,574
Book on Dr Slaa's history in offing | The Citizen

(Kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Ibara ya 18(2):

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa kutumia Haki yetu ya Kikatiba, “ Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za Wananchi, na pia juu ya maswala muhimu kwa jamii”(Katiba 18(1) mimi Balozi Dr Willibrod Peter Slaa pamoja na ndugu RoseMary Mwaitwange, George Mwaipungu na Juma Kaswahili, kwa niaba ya SAUTI YA WATANZANIA, tumeona tuzungumze kuhusu maswala yanayoihusu Taifa letu.

Ndugu Wanahabari na kwa njia yenu, naomba ieleweke bila chembe yeyote ya Wasiwasi kuwa Taarifa hii haina dhamira yeyote ya kupinga Uwekezaji wa kweli na wenye tija kwa manufaa ya Taifa letu na hasa uwekezaji wenye kulenga kuwanufaisha Watanzania kwa ujumla, Watanzania wa Pande zote mbili za Mwungano yaani Tanzania Bara ( Tanganyika) na Tanzania Zanzibar. Hivyo ninatoa tahadhari kuanzia mwanzo kuwa si nia wala lengo la Taarifa hii kupinga uwekezaji wowote wenye tija, uwekezaji usio na hila. Ninapinga na tunapinga kwa nguvu zetu zote chochote kinachofanyika katika katika misingi ya Giza iwe uwekezaji au vyovyote vile.

Baada ya Tahadhari hiyo niseme kuwa hivi karibuni kumekuwa na minong’ono na Taarifa katika mitandao mbalimbali kuhusiana na uwekaji Saini mikataba mbalimbali yenye kutia mashaka. Kwa mtu yeyote mwenye nia njema na Taifa hili na mwenye kutambua wajibu wake wa Kikatiba kuwa “ kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asili ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, mali ya mamlaks ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine” , ni jukumu letu sote, Mimi, wewe Mwandishi wa Habari, mwananchi wa kawaida yaani mkulima, mfugaji, mfanyikazi, viongozi wa madhehebu ya dini. Kwa kifupi kila mmoja wetu labda isipokuwa watoto wachanga; na wazee ambao kwa vigezo vyote wamechoks kabisa.

Huu ni wajibu wetu sote. Kwa bahati mbaya Watanzania wengi tumebaki kuwa Watazamaji wakati “ Mali zetu” katika sura zake mbalimbali zikitapanywa, tena mara nyingi na “ wale tuliowapa dhamana ya kuzisimamia. Watanzania tumekuwa kama mkulima aliyehangaika kuiandaa shamba lake kwa nguvu na jasho kubwa, akalima na kupanda lakini akaachia kwale kufukua mbegu na kuzila, na hata pale zilipoota na kukua akaachia Nyani kutafuna mahindi yake yote.

Kwa maelezo yeyote yale huyo ni mkulima mzembe, asiyethamini hata jasho lake mwenyewe na hatimaye akilia pale anapokuwa ameingia kwenye kilindi kikubwa cha umaskini. Ni dhahiri yote hayo ni kutokana na Uzembe wake.

Ndugu Waandishi wa Habari, leo tunapozungumza nanyi tulichokiita minong’ono tena kwani swala liliingia Bungeni na Azimio rasmi kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo 10 Juni 2023. Azimio hili lilihusu maswala hasa ya Uwekezaji kupitia kinachoitwa Azimio la kurithia Mkataba IGA.

Nitataja tu baadhi ya maeneo ya mchakato huo wa uwekezaji kama vile MOU ( Memorandum of. Understanding) inayosemekana kusainiwa baina ya Oman Investment Authority ( OIA) na Serikali ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, kuhusiano na uwekezaji unaotarajiwa kufanyika katika nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro. Uwekaji Saini Mkataba huo ulifanyika Tarehe 13/06/2022 saa 10.08 ( 4.08 PM), wakati wa Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan nchini Oman.

Katika picha inayomwonyesha Mhe.Dr. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, na Kiongozi wa Oman, Sami Al Sinani, Senior Manager-logistics and Infrastructure at OIA). Mhe Rais Samia anasemekana alishuhudia uwekaji huo ( Picha zimepigwa na Joseph). Pamoja na kusainiwa kwa Mkataba huu kuhusu KIA, mikataba mingine ilihusu pia MOU kati ya OIA na Zanzibar Investment Promotion Authority. Hadi muda huu tunapozungumza nanyi Serikali yetu haijatoa Taarifa ya aina yeyote ile kuhusiana na Makubaliano hayo.

Hata hivyo, taarifa kwenye mitandao ya kijamiin inahusu Mkataba unaoonekana kusainiwa Tarehe 23/04/2022 saa12.18(6.18PM) mkataba unaosemekana kuwa na Thamani ya US$ 7. Trillion lakini hakuna Taarifa za kina. Ninapenda kuamini kuwa hii ni mikataba ya kibiashara na hakuna MOU inayoonekana wala IGA zilizosainiwa. Swala la msingi hapa kwa wale wenye kumbukumbu ni kuwa Wananchi tunaofahamu wajibu wetu wa Kikataba tunatambua jinsi Taifa letu lilivyoumizwa na ufisadi uliofanyika Ndani ya Taifa letu kupitia Mikataba Mibovu.

Mikataba hiyo ni kama, “From Big Scandals to Funerals, the 10th Parliament saw it all” ( Rejea The Citizen, Thursday, July 09, 2015-updated 20th April, 2021), Richmond, Symbion, IPTL/ VIP Engendering SAGA, Operation Tokomeza in response to Parliamentary Committee on Lands,Natural Resources and Tourism. The 10th Parliament’s handling of mega scandals exposed through strong opposition, forced president Kikwete to sacked 4 Cabinet Ministers).

Mgogoro Mkubwa Uwekezaji Loliondo ( Ortello Business Corporation( OBC) na athari zake kwa Wananchi wa Loliondo). Kwa Bahati mbaya, kutokana na uchaguzi wa “Kiinimacho” wa 2019/ 20 Taifa letu limegeuka kuwa “ a de facto one Party State”. Hivyo hata pale panapokuwa na matukio makubwa yanayotafuna Taifa letu hakuna tena Sauti “ itokayo nyikani” japo kuwajulisha wananchi yanayojiri. Kwa vile Rais wa Jamhuri ameonekana akishuhudia uwekaji saini mikataba hiyo, ilikuwa busara ya kawaida Taifa kuarifiwa juu ya mikata hiyo. Sisi sote ni mashahidi kuwa Tanzania ina Takriban Kata 3,337, Vijiji 12,423, Mitaa, 3,741 ( Tovuti TAMISEMI).

Katika uchaguzi wa 2019 na 2020 Viongozi hao wote “Walichaguliwa” katika Mfumo wa Uchaguzi ambao unapatikana tu Tanzania ( Made in Tanzania) na hivyo karibu wote wanatoka Chama cha Mapinduzi. Matokeo yake, ni “ Total Collapse” ya Mfumo wa Uongozi na Utawala. Leo takriban Miaka 3 tangu uchaguzi katika Vijiji asilia 99 Taarifa ya Mapato na Matumizi inayopaswa kusomwa katika Mikutano Mikuu ya Vijiji na Mitaa haijasomwa.

Wakati huo huo Wananchi wakipiga kelele kuwa kuna “ upigaji mkubwa kila Mahali” , jambo ambalo limeangamiza “ Maendeleo” katika ngazi hiyo Muhimu sana ya Uongozi. Serikali ya CCM wakati ikihangaika “Siasa za Uhai“ wake imeweka pamba masikioni na Kilio hicho cha Wananchi kinaelekea kupeperushwa bila kiongozi yeyote mwenye dhamira ya kutaka kuwasaidia. Hivyo, ukiunganisha hayo yote, hakuna njia Nyingine, Ni lazima kila mmoja wetu, wananchi wote katika ujumla wao kupitia vijiji vyao, Mitaa yao, vitongoji vyao Lazima tupige kelele ili kuokoa Msendeleo yetu( Kat.Ibara ya 27(1)(2).

Ndugu Waandishi wa Habari, nikirejea kwenye swala la MOU na “ Intergovernmental Agreement” hili si jambo geni nchini Tanzania. Kwa wale wasiofahamu kwa lugha rahisi. MOU ni “ Memorandum of Understanding” ni “makubaliano ya awali” ambayo pande mbili zinazotaka kuingia kwenye Mkataba na kwa kawaida Serikali moja na nyingine zina saini. MOU hufuatiwa na Mkataba Unaoitwa InterGovernmental Agreement kwa. Kifupi IGA. Hivyo mkataba huu tunaopigia kelele si wa kwanza kwa Serikali ya Tanzania.

Ndugu Waandishi wa Habari, ninapenda kurejea kuwa Mikataba ya kiuwekezaji ambayo Taifa letu imesaini na Nchi mbali mbali ni mingi. Hata siku moja Watanzania hatujawahi kulalamika wala kupiga kelele kama sasa. Labda kwa Taarifa yenu, Bilateral Investment Treaties yaani Mikataba ya kiuwekezaji iliyosailiwa Baina ya Tanzania na Serikali Nje ni kama Ifuatavyo:

Jumla ya BITS ni 2,829
Inayoendelea kutumika. 2,219
Yenye Maslahi ya Kibiashara. 435
Inayotumika. 264

Ndugu Waandishi wa Habari, ni dhahiri kama mnavyoona, Tatizo siyo kwamba Watanzania tunapinga Uwekezaji, wala kupinga Mkataba wa Uwekezaji. Hivyo mkiona tunapiga kelele kupinga MOU na IGA hii inayohusu DP World ni vema Watanzania wakapata uelewa na kufahamu madhara ya kina kuhusiana na Mkataba unaolalamikiwa.

Ndugu Waandishi, napenda kuwakumbusha kuwa Mradi wa DP Workd ni moja kati ya Mikataba 17 iliyosainiwa wakati wa Dubai Expo 2022. Tatizo kubwa na la msingi sana ni usiri mkubwa uliolikumba mchakato mzima wa MOU hii na baadaye IGA. Makubaliano ya Awali. ( MOU) yalisainiwa tarehe 28 Februari 2022 baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Tanzania ( TPA) na Kampuni ya DP World inayomilikiwa na Serikali ya Dubai ( The Emirate of Dubai).

Aidha, Tarehe 25 Oktoba Mkataba yaani Intergovernmental Agreement( IGA) ulisainiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai. Ndugu Waandishi, kabla sijaujadili Mkataba wenyewe, nataka kutamka kuwa tangu kusainiwa MOU 28 February na baadaye IGA hapakuwa na Taarifa yeyote rasmi, wala na Mhe. Rais, wala na Mhe. Waziri hasa kwa kuzingatia uzito wa Mkataba huu.

Ni dhahiri si Mhe Rais wala Mhe Waziri mwenye dhamana aliyeona uzito wala umuhimu wa kutoa Taarifa kwa umma pamoja na kuwa Mkataba huu unagusa maswala mapana ya Taifa letu na kuleta mabadiliko makubwa sana katika Sheria zetu. Aidha inawezekana kati ya Mhe. Rais na watu wake hakuna aliyoona madhara makubwa ya Mkataba waliouanzisha.

Ndugu Waandishi wa Habari, Kwa ufupi sana kabla ya Kujadili iGA ya DP World, ni muhimu tujikumbushe Miradi kadhaa ya Uwekezaji ambapo tulisaini Mikataba mbalimbali na jinsi Taifa halikufaidika na uwekezaji huo, siyo tu kwamba hatukufaidika na mikataba hiyo ya Uwekezaji, bali kwa uzoefu huo tunatafakari ni nini leo kinatuhakikishia IGA hii ya DP World itatunufaisha kama tunavyotaka kuaminishwa?

Mradi wa kwanza ni mradi wa “ Lease Contract baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya Biwater Gauff (Tanzania). Kampuni ilikuwa na Mkataba wa kuwekeza katika Mradi mkubwa wa Maji katika mji wa Dar es Salaam, Pwani na Bagamoyo.

Badala ya Tanzania kunufaika na uwekezaji huo, mgogoro baina ya Kampuni ya Biwater na Serikali ya Tanzania uliishia katika mahakama ya International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID case no ARB/05/22). Japo Serikali ya Tanzania ilishinda Shauri hili, lakini kiasi kikubwa cha Fedha zilitumika kulipa gharama za Shauri. Aidha muda mwingi ulipotea kwenye Shauri badala ya kutoa huduma ya Maji kwa Wananchi.

Mradi mwingine ambao ningelipenda kuuelezea ni Mkataba wa Uendeshaji wa “ Utility Management Contract” baina ya shirika la Tanesco na Kampuni ya Afrika ya Kusini ya Netgroup Solutions ( Rejea MIR Working Paper, March 2007, Rebecca Ghanadan- University of California Berkeley).

Katika Mikataba ambayo imesumbua Serikali yetu ni Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd. Pamoja na kuwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd, ni Mkataba ambao umeleta maumivu makubwa katika Taifa letu bila kufikia malengo ya kimaendeleo yaliyotegemewa. Huu ndio mradi ambao hatimaye, ulihusisha Rushwa kubwa ambayo iliwagusa viongozi wakubwa wa Dini, viongozi ws Serikali wakiwemo Majaji ( Rejea ICSID case no ARB/98/8 final judgement 22/06/2001.

Ndugu Wanahabari, katika Mikataba ya uwekezaji pengine hakuna Mkataba ambao umefeli kama Mkataba baina ya Shirika la Reli la TRC na Kampuni ya India ya Rites. Mkataba huu ulihusisha Shirika la Kimataifa la International Finance Corporation ( Project no 25151, Date SPI disclosed – June 22, 2007, Approved July 26th, 2007 na kusainiwa 2007 na uwekezaji kuanza 11 June,2008). Mkataba huu ulihusu Uwekezaji wa kuendeleza, ukarabati (Rehabilitation), kukuza ( develop), na uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania yenye jumla ya Km 2,700 kwa gharama Us $ 44 Millioni.

Mkataba ulikuwa kwa utaratibu wa “Concession”. Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania uwekezaji huo ulisimamiwa na Presidential Parastatal Sector Reform Commission of the Government of Tanzania ( PSRC).

Ndugu Wanahabari, wote mnafahamu kuwa Mkataba huo uliosainiwa 3 Septemba 2007, na kuanza kazi 1 Oktoba 2007 Serikali ya Tanzania kupitia TRL ikimiliki asilimia 49 ya hisa. Kutokana matatizo mbalimbali ikiwemo kutokuwemo na uwezo, udanganyifu. Mkataba huo ulivunjwa hatimaye Mwaka 2010 ( The Citizen, June, 10,2010- Thesis “ Viability of a public Private Partnership, A case of Railway Concession in Tanzania”, Alex Shlfyk, ).

Kwa ujumla tafiti mbalimbali zinaonyesha Matatizo makubwa, yanayopelekea Mikataba mingi kuvunjika yanatokana na matatizo ya kimkataba, usiri mkubwa katika mikataba inavyoandaliwa, kukosekana umakini katika maandalizi na usimamizi wa utekelezaji wa Mikataba husika. Huu ndio msingi mkubwa wa hofu kubwa katika mioyo na vichwa vya Watanzania kuhusiana na IGA hii kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano na DP World ya Serikali ya Emirates.

Kwa mtu yeyote makini atatambua kwanini Watanzania tuna Hofu kubwa na Mkataba hasa kutokana usiri mkubwa lakini pia ushabiki mkubwa wakati unajadiliwa na Bunge la Jamhuri ambalo kimsingi ni la Chama Kimoja.

Ndugu Wanahabari, Mfano wa Mwisho ambao Waandishi wengi ambao Waandishi wengi mnaufahamu ni Mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni iliyokabidhiwa “ Hunting Block” ambapo Mwekezaji Kampuni ya Dubai ilikabidhiwa eneo bila kuzingatia mahitaji wa Wananchi wa asili katika eneo la Loliondo mwaka 1992. Sote tunafahamu jinsi Uwekezaji huo ulivyowaathiri ndugu zetu Wananchi wakazi wa Loliondo, ambapo nyumba zimechomwa moto, damu ya wakazi kumwagika katika kupambania haki zao.

Lakini Serikali ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania inayoongozwa na CCM imeweka “pamba masikioni”.( Rejea Citizen, “ Why the Loliondo Controversy refuses to go away, Citizen, Thursday 23 June, 2022).

Ndugu Wanahabari, baada ya kuonyesha jinsi Taifa letu “lilivyopigwa” katika Mikataba mbalimbali ya Uwekezaji. Niruhusuni sasa niweze kufanya uchambuzi mdogo wa Azimio lililowasilishwa Bungeni kwa Mujibu wa Special Supplement, No 11 ya 31 March, 2023. Azimio hilo limewasilishwa kwa Mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 110 (1) na 110(2).

Aidha, napenda kuweka wazi, Si nia yangu kupinga Uwekezaji, wa aina yeyote, mkubwa au Mdogo wenye nia na lengo la kuendeleza Taifa letu, na hasa unaolenga kuwanufaisha Watanzania katika Umoja wetu. Ieleweke wazi tunapinga ni namna tunavyoletewa uwekezaji ambao hauna Tija kwa Taifa letu na Wananchi wake kwa ujumla na hata moja moja. Ninachokataa, ni aina ya uwekezaji isiyoeleweka katika mantiki na hata maudhuinyake, au iliyofumbwa fumbwa kama ambavyo nimeonyesha kwenye mifano iliyotangulia hapa juu.

Mtakumbuka, Azimio liliwasilishwa Bungeni siku ya Jumamosi, Tarehe 10 Juni, 2023 kwa hotuba ya Waziri wa Ujenzi naUchukuzi, Prof. Mbarawa Makame.

“ Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya kuridhiwa makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023 ( Intergovernmental Agreement- iGA), Between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai Concerning economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania”
……” Kwa kuwa serikali ya Jamhuri..” ( Hotuba ya Waziri Prof. Mbarawa, Mp)

Ndugu Waandishi wa Habari, kabla ya kufanya uchambuzi ningependa kuweka maelezo mafupi kuhusiana na mchakato hadi kufikia hatua ya Azimio hili kurithiwa na Bunge. Ikumbukwe kuwa, Makubaliano ya Awali Memorandum of Understanding- MOU) ilisainiwa tarehe 28 Februari, 2022 baina ya TPA (Mamlaka Ya Bandari Tanzania na Kampuni ya DPWorld. Shughuli ya uwekaji saini ulishuhudiwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , akiwa Dubai wakati huo kwa Dubai Expo 2022.

Makubaliano hayo yalikuwa na lengo la kubainisha maeneo mahusisi ya Ushirikiano ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundo mbinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa Makuu, maeneo maalum ya kiuchumi( Special Economic zones), maeneo ya maegesho na utunzaji mizigo ( logistic Parks) na maeneo ya kanda ya kibiashara ( Trade corridors). Mhe. Rais, baada ya kurejea nchini , licha ya Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu, hakugusia, japo kutaja tu kuwa kuna mkataba wa uwekezaji mkubwa umesainiwa.

Ndugu Waandishi, hatua ya Pili ni “ kusainiwa” kwa Mkataba. ( Intergovernmental Agreement - IGA). Mkataba huu ulisainiwa na Serikali ya JMT na Serikali ya Emirates Tarehe 25 October, 2022. IGA imesainiwa kwa upande wa Tanzania kwa mamlaka ya Rais Samia

(Instrument of full Powers: I Samia Suluhu Hassan, the President of the URT, do Hereby AUTHORIZE AND EMPOWER ,Hon.Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, Mp, Minister for Works and Transport, While in Dodoma Tanzania to sign on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania and the Government of Dubai concerning economic and Social Partnership for the Development and improving performance of Sea and Lake Ports in Tanzania Done at Dodoma, Tanzania On this 3rd day ofOctober, year Twenty and Twenty Third ( signed by …… President Of URT). Kwa Upande wa Serikali ya Dubai Appointment Letter ilitolewa na A.E Ahmed Mahboob Musabih to act in the name and on behalf of the Emirate of Dubai na kusainiwa ( Zimeambatanishwa)

Baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kwa mujibu wa mamlaka ya Kif. 25 cha IGA, shughuli za awali za utekelezaji – “yaani early project activities zitaanza ikiwa ni pamoja na kujenga barabara za kufika eneo la mradi. Taarifa ya Kamati ya Pamoja ya Bunge, para1.2) . Hadi wakati huo tukumbuke kuwa Taifa na Watanzania walikuwa hawajajulishwa wala kupewa Taarifa yeyote ile inayohusu Mkataba mkubwa wa Uwekezaji, unaohusisha siyo tu Mkataba wa kawaida wa kibiashara bali, uwekezaji baina ya Jamhuri ya Muungano na Kampuni inayomilikiwa na Uongozi wa Nchi ya Dubai ( ambayo ni sehemu ya Falme za UAE……Emirates).

Hata hivyo naomba kuwakumbusha kuwa pamoja na mkataba huu, Katika Dubai Expo 2020 Serikali ya Tanzania iliyowakilishwa na Mhe. Rasi Samia. Kulisainiwa Mikataba mingine 17 ambayo hadi tunaposungumza haijatolewa Taarifa ya aina yeyote ile. Waliohudhuria Maonyesho ni Viongozi wa Serikali; wamesafiri, wamelala Hoteli, na wamekula Chakula kwa Kodi ya Watanzania. Ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa awananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii linanilazimisha kuwakumbusha uhitaji na upatikanaji wa haraka wa Katiba mpya. Tungelikuwa na Katiba Mpya na bora haya yasingelitokea na kama yangelitokea kutokana na uwepo wa Vyombo vya kuwajibishana,

Mkataba huo ( IGA) inatamka kuwa “ Mchakato wakuridhia Mkataba utaanza ndani ya Siku 30 mara tu baada ya kusainiwa Mkataba. Lengo ni kufanya masharti ya Mkataba kuzibana pande husika chini ya Sheria ya Kimataifa yaani “to make this a binding obligation of each State Party under the International law)”. Lakini sisi sote ni Mashahidi kuwa hata katika hatua hiyo wala Taifa halikujulishwa kwa namna yeyote ile mpaka Taarifa ilipovuja.

Swali muhimu, ni kuwa kwa vipengele cha Mkataba siku 30 kama nilivyotaja hapo juu ( Taarifa ya Kamati Kif.1.2) kiliisha kumalizika, Kwa maneno mengine Mkataba uwe umeridhiwa ndani ya Siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takriban 8. Kwa hali hiyo, tuna uhakika gani kuwa Tanzania ina uwezo wa kutimiza masharti ya Mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza ucheleweshaji huo mkubwa. Ni dhahiri kuwa kwa hali hii hatuwezi kuwa na uhakika kutimiza masharti ya utekelezaji huu jambo ambalo litatuingiza siyo tu kwenye matatizo makubwa bali pia kwenye gharama kubwa. Sitaki kuwa nabii!

Azimio hilo lilijadiliwa na Bunge , kwa msingi wa Kanuni ya Bunge Kif. 110 na kuamuliwa kwa utaratibu unaowekwa na Kanuni ya 111. Kanuni hiyo inaweka Msingi wa kujadili Hoja ambapo mjadala utahusu, “ Masharti ya mkataba husika”. Aidha, uamuzi wa Bunge utakuwa na Mambo 3 yaani 111(2(a) Kuridhia Masharti yote ya Mkataba, 111(2)(b)kuridhia baadhi ya Mkataba iwapo Mkataba unaruhusu kufanya hivyo; au 111(3)(c) kukataa kuridhia mkataba husika. Hata hivyo Azimio hilo zito lilijadiliwa kwa Saa takriban 8 tu na Kupitishwa kwa utaratibu wa Kanuni ya 111(2)(a) yaani ilipitishwa kwa kauli ya “Ndiyo” kwa kuridhia Masharti yote ya Mkataba. Ndio kusema Bunge letu halikuona vipengele tata ndani ya Mkataba, ikiwa ni pamoja na vile vinavyopingana na Sheria yetu “ The National Wealth Resources, 2017“.

Ndugu Waandishi, japo kuna maeneo mengi yenye utata, hata hivyo kwa ajili ya muda nitajikita katika maeneo yafuatayo:

1) Mkataba huo Kif. Cha 1 inaweka Msingi wa kisheria unaofunga pande husika katika Ushirikiano. Ushirikiano huu ni baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World, inayomilikiwa na Mfalme wa Emirates, hivyo ni Mkataba baina ya Serikali ya Emirate of- Dubai ( ambao) ni sehemu ya united Arab Emirates na Serikali ya Tanzania. Hivyo ni utawala wa kifalme ( Absolute Monarchy) , maamuzi ya Mfalme ni ya mwisho na hivyo hahitaji idhini ya mtu yeyote katika maamuzi yake. Tanzania ni Jamhuri na Inaongozwa na Katiba na Sheria zilizopitishwa na Bunge. Hivyo Kampuni ya DP World ni Kampuni ya Serikali ya Emirate of Dubai.

Mkataba huu unazifunga pande zote mbili zilizoko kwenye Mkataba. Mkataba unahusu kuendeleza, kuboresha, kuendesha na kusimamia maswala ya Bandari katika bahari, Maziwa, Maeneo yote yaliyotengwa kwa shughuli za uchumi, logistic Parks, njia zote za Biashara, na meneo yote muhimu ya miundombinu ya Bandari ndani ya Tanzania ( cooperation for the development, improvement,management mand operation of sea and lake ports, special economic Zones, logistic parks, trade corridors and other related strategic port infrastructure in Tanzania.

Hapa ndipo linapoanza Tatizo la kwanza. Mkataba Yaani IGA inagusa maeneo yote muhimu ya Tanzania ambayo mwaka 2017 yalitungiwa Sheria Maalum ya “ The Natural Wealth and Resources( Permanent Sovereignity) Act, 2017. Pamoja na Mengine, Sheria hiyo inatamka bayana kuwa “ The People of The United Republic of Tanzania SHALL have Permanent Sovereignity over all Natural wealth and Resources. Sect.4(1). The ownership and control over natural resources shall be exercised by and through the government on behalf of the People and the United Republic Sect.4(2) .

This goes up to Section 4(3-5). Ni wazi dhamira ya Sheria hii kuhifadhi ns kulinda Rasilimali hizi muhimu ipo wazi. Ni kweli Kifungu cha 5(2) kinasema kuwa “ The Natural Wealth SHALL be held in Trust by the President on behalf of the People of the United Republic”.

Hivyo Rais na Serikali wanazisimamia Rasilimali hizi kwa niaba ya Wananchi, na hivyo Wananchi Wanahitaji “ Kushirikishwa” katika maamuzi yeyote makubwa na Mazito. Ikumbukwe kuwa, hata “Public Hearing” ambayo kwa taratibu zetu ingelikuwa njia ya kuwashirikisha Wananchi katika kutoa maoni yao kwa Kamati ya Bunge iligubikwa na figisu, kwani mtakumbuka Tangazo la Mwito kwa wananchi kushiriki kwenye Public hearing ilitolewa Tarehe 5 June, 2023 Wananchi wakitakiwa wahudhurie Public Hearing Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Dodoman 6Th June, 2023 yaani watoke kona zote za Tanzania na wafike Dodoma ndani ya saa 24.

Hi ni kiasheria ya wazi kuwa Serikali na vyombo vyake Havithamini, na wala havitambui kuwa Rais ni “ Mdhamini” na Hivyo maoni ya wananchi, tena kwa uwingi yanahitajika. Ingeliwezekana Maoni hayo yalitakiwa yakusanywe kwenye Vijiji kupitia Serikali zao za Vijiji na Mitaa kama ilivyofanyika wakati wa Serikali ya Awamu ya kwanza ambapo maoni yalitolewa kutoka Taifa hadi kijijini na Maoni hayo kurudi kutoka Kijijini hadi Taifa. Hii ndio maana na Tafsiri halisi ya “ wananchi kuwa na Mamlaka”.

Kilichofanywa na Bunge ni Kichekesho na kuvunja Sheria, dharau kwa Wananchi ambao ndio “ Wamiliki wa Rasilimali zote ndani ya Nchi”. Labda mfano mzuri ni “ Mchungaji aliyekabidhiwa kuchunga Kondoo kutumia nafasi yake kuchinja na kula Kondoo aliokabdhiwa huko huko Machungani.

Aidha, ikumbukwe, kuwa Serikali iliyoko, ina “ Legitimacy” ya wasiwasi kutokana na Uchaguzi wa 2019 na 2020 “ kuvurugwa kwa Makusudi” na Chama cha Mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye Macho na akili hahitaji kuambiwa kuhusu hilo na Waandishi nyote ni Mashahidi. Kwa matokeo hayo Bunge limefanywa kuwa chama kimoja na hivyo kukosa “ Legitimacy” ya kufanya maamuzi makubwa kuhusu Rasilimali za Nchi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha IGA, inatamka wazi kuwa Rasilimali zote kama zilivyotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya nchi ya Kigeni bila dalili yeyote ya tahadhari ya ulinzi wa Taifa. Nitumie fursa hii kutoa mfano mwaka 1997 wakati Serikali ya Awamu ya 4 ilijaribu kubinafsisha Mashurika muhimu ya Taifa ya Bandari, Uwanja wa Ndege na Shirika la Air Tanzania, Shirika la Umeme ( TANESCO), Shirika la Simu ( TTCL). Wakati tukiwa kwenye Kamati ya Bunge alikuja kilngozi moja kutoka Shirika moja akatupa tahadhari ifuatayo “ Waheshimiwa Wabunge, katu msikubali hayo mashirika kubinafsishwa kwani ni muhimu sana kwa ‘ USALAMA wa Taifa letu”.

Kiongozi huyo akatueleza jinsi wakati wa Vita vya Nduli Idi Amin, sehemu kubwa ya Mkoa wetu wa Kagera ulikuwa unapigwa mabomu na sehemu kubwa hasa maeneo ya mutukula kutekwa, Mwalimu alitangaza “ Kuwa Tuna Sababu ya kumpiga adui, Nia tunayo na uwezo tunao”. Wananchi waliitikia na kuhamasika sana. Walichangia kwa kuruhusu vijana wao askari na Mgambo kwenda vitani, walichangia fedha na wanyama kusaidia chakula cha Wapiganaji wetu na wenye Magari walitoa magari yao. Tatizo likawa Mafuta.

Ikumbukwe tulikuwa na Kampuni ya Mafuta ambayo Tanzania tulikuwa tukimiliki asilimia 51 na Mbia wetu kutoka nchi mojawapo Rafiki aliweka ngumu kutoa mafuta kwa maelezo kuwa “ yeye ni mbia wetu, lakinin tunayeenda kupigana naye pia ni rafiki yake. Hivyo hayuko tayari kutoa Mafuta kupeleka askari na vifaa Mkoani Kagera”. Kwa karibu siku 5 Askari wetu, vifaa havikuweza kuondoka kwa kukosa nafuta, wakati bohari ilijaa Mafuta. Mwl Nyerere akapaswa kufanya kazi ya ziada kupata mafuta.

Wabunge tulielewa sana athari ya ubinafsishaji na ndio maana leo Serikali ya Awamu ya 6 imeyakuta mashirika hayo, hata kama siyo imara ambavyo tungelitamani pyawe. Leo, Rais, ambaye ni mdhamini kwa niaba ya Wananchi, Anabinafsisha Bandari zote za Bahari Kuu, Maziwa yote, na popote Bandari zilipo; “anabinafsisha” Viwanja vya Ndege, Reli , na Miundombinu yote muhimu! Kuingia mkataba na Kampuni za Ujenzi.

Lakini kuyaweka yote chini ya Kampuni moja, tena Kanpuni ya Serikali ya kigeni! Jambo hilo linahitaji kutafakariwa tena na kutazamwa upya. Hayo yamefanywa wakati wananchi kwa makusudi tumenyinwa fursa ya kutoa maoni yetu kwenye Kamati. Isitoshe, hata wakati Wa mjadala Bungeni mjadala ulijaa vijembe, na kejeli kana kwamba nchi hii ni mali ya Chama fulani! kabla hatujapewa maelezo ya kuridhisha kuhusu usalama wa Taifa letu. Hili kwa maelezo yeyote. Jambo hili linatia shaka kuhusu usalama siyo tu wa Rasilimali zetu, bali usalama wa Taifa.

Ndugu Waandishi, inawezekana wengine wenu hamkumbuki yaliyotokea kwa majirani zetu Uganda. Sijui wangapi wanakumbuka tukio la “ Entebe Raid” ambapo wapiganaji wa Popular Front for Liberation of Palestine waliteka ndege ya Air France na kutua Entebe wakati wakitafuta eneo salama kwao.

Ndani ya ndege kulikuwa na Abiria wa Israel, Katika kilichoitwa “Operation Thunderbolt” Jeshi la Israel lilifanikiwa kuwakomboa “Raia” wao ndani ya muda mfupi sana, Tarehe July 3 na July 4 July 1976. Kazi ya kuwakomboa Abiria wao( pamoja na wengine) , iliwezekana bila mauaji kwa kuwa Uwanja wa Ndege wa Entebe ulijengwa na Kampuni ( ya kijeshi ) ya Israel. Hivyo walijua Ramani na mpangilio wote wa Uwanja wa Entebe. Hiyo ilirahisisha kutua na kuvamia bila “ Jeshi la Uganda kujua kilichotokea.

Wanajeshin hao wa Israel walifika na kufanya “ukombozi” wa abiria wasio na hatia kutokana na Ramani za Uwanja na miundombinu ya uwanja huo ambayo walikuwa wanaijua. Naamini, kuepuka t ukio kama hilo ndio maana Ujenzi wote wa Ikulu ya Dodoma umefanyika na vijana wetu wa Jeshi la Wananchi, kuanzia michoro, hadi ujenzi wenyewe. Nadhani Serikali ilifanya uamuzi huo kutokana na uzoefu huo wa “.Operation Thunderbolt”

Ndugu Waandishi, jambo la pili lililonistua mpaka kuchukua hatua hii ya Kuitisha Press Conference, ni Uvunjifu Mkubwa wa Katiba unaanza kuwa jambo la kawaida katika nchi yetu. Katiba yetu, Ibara ya 4 inasema, “ Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa Madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara hii ( Ibara 4(1-3), kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya kwanza iliyoko mwisho wa Katiba hii; na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo mambo ya Muungano ( Katiba Ibara 4 (3). Ukitazama Nyongeza ya Kwanza ya Katiba Bandari ni namba 11 katika Listi ya Mambo ya Mwungano.

Aidha, katika Nyongeza ya Pili, Orodha ya Kwanza na hata Orodha ya Pili Bandari siyo Jambo lisilo la Muungano na hivyo halipo katika Mambo ya Zanzibar. Aidha Sheria, The Ports Act, 2004, inasomeka , “ This Act shall apply ( siyo “May”) to Seaports and inland waterways ports in mainland Tanzania and Zanzibar( sect.2(1). Kwa upande mwingine, Zanzibar nako kuna Sheria ya The Zanzibar Ports Corporation Act, 1997. Huu ni mkanganyiko wa wazi katika Katiba yetu.

Ni wazi haya ndiyo baadhi ya mambo yanayofanya Madai ya Katiba Mpya, na Katiba Mpya ipatikane sasa siyo kesho. Ni kwa msingi huo, Katiba ya Mwungano itaangaliwa ni wazi kuachwa kwa Bandari za Zanzibar linaleta taharuki . Na Kinaleta dhana ya Ubaguzi. Ni muhimu mgongano baina ya Katiba hizi mbili ukarekebishwa haraka sana kuondoa Mkanganyiko huu unaoweza kuleta dhana nzima ya Ubaguzi kwa wananchi wasio wanasheria.

Ndugu Waandishi, Kifungu cha 5 cha Mkataba ( Article 5 of IGA) kinatoa mamlaka na haki zote ( Exclusive Rights) kwa DP World kukuza ( develop) na kuendesha ( Manage) na kutekeleza ( Operate) miradi yote kama ilivyoonyeshwa kwenye Appendix 1, awamu ya kwanza.

Mkataba pia unaeleza kuwa utekelezaji wa Mradi/ Miradi utafanyika mara tu baada ya kusainiwa kwa mikataba mbalimbali itakayoandaliwa kwa mujibu wa IGA. IGA ilisainiwa Tarehe 28 Oktoba, 2022. Leo ni takriban miezi 8 lakini hadi Azimio la kuridhia lilipowasilishwa Bungeni Tarehe 10 Juni, hakuna Mikataba mbalimbali iliyowahi kufanywa na DP World kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha IGA.

Inashangaza Bunge lilijadili nini kama halikuweza kujadili na hata kuhoji maswali ya wazi kama hayo, badala yake kulikuwa na mijadala iliyojikita katika ushabiki wa kisiasa, kubeza vyama ambavyo wala havikuwa Bungeni na hivyo kuwa na fursa ya kujibu mapigo na au kutoa mchango wao kwa manufaa ya Taifa. Hayo ni madhara ya Siasa ya 2019/ 20 ambayo iliwanyima Watanzania fursa ya kuwa na Upinzani wa kuaminika ndani ya Bunge. Ushabiki na uharamia wa siasa mbovu ya 2020 sasa ndio unalitafuna Taifa.

Anayeathirika ni Taifa na kwa namna moja au nyingine, wananchi moja kwa moja kwa kukosa fursa ya kutoa mchango wao katika Chombo hiki kikuu katika Utawala Bora katika Nchi yetu. Wananchi kwa ujumla wetu ni lazima tuamke na kupiga kelele, kila moja peke yake au katika makundi ya kisiasa, au vyama vya Hisri NGO, vyama vya Wafanyi Biashara ( Ninawapongeza Wafanyibiashara wa Kariakoo waliopaza Sauti yao hivi karibuni kudai haki zao), Madhehebu ya dini, Vyama vya Siasa vya Upinzani nao katika mapambano ya kulikomboa Taifa havina budi kutoa “Leadership” hasa kwa kuzingatia historia ya Taifa letu.

Hii nchi ni yetu sote, “ tukicheka na nyani tutavuna mabua”. Nadhani nimeeleweka. Kwa kweli inasikitisha kama Bunge liliisha kupata Taarifa kidogo sana ( very scanty) Limeridhia Azimio katika Misingi gani. Nashauri Watakaorudi kwenye Majimbo yao, Wabunge hao wapate kibano Ili waeleze ni kitu gani hasa waliridhia, au waliona Maelekezo waliyopewa na Chama chao kwenye ‘Party Caucus’ pale Ukumbi wa Pius Msekwa yalikuwa muhimu zaidi kuliko Maslahi ya Taifa!

Ndugu Wanahabari, Uwekezaji wa DP World sio wa kwanza Tanzania. Ukiacha uwekezaji wao Somaliland ( nchi isiyotambulika rasmi- breakaway toka Somalia) Djibouti, Namibia, Mozambique, maeneo mengi kumekuwa na migogoro inayohusisha Rushwa. DP World inao uwekezaji pia marekani na Ulaya ya Magharibi. Utafiti unaonyesha kuwa kwa Marekani na Canada DP World imeingia kwenye Mikataba na nchi hizo kama Kampuni na siyo kama Serikali ya Dubai.

Ni lazima tujiulizev kuna nini hapa. Kinachoonekana ni kuwa wenzetu wako makini sana katika Maandalizi ya Mikataba yao. Tunayo mifano ya DP World Callao/ Peru, DP World lima, DP World Datos. Hii ina maana ya kuwa kila eneo kulikuwa na Makubaliano tofauti lakini hakuna Makubaliano ya Kubinafsisha Bandari zote za Peru kwa Mkataba moja. Isitoshe Mikataba unahusu jambo mahususi mathalan, Container Terminal. Vivyo hivyo kwa Mikataba ya Vancouver Canada, ambapo mikataba ilikuwa ikihusu Berths/Terminals, port operation. Mifano ni Mikataba ya Vancouver, Prince Rupert,Fraser Surrey.

Jambo la pili ni kuwa Mikataba yote ilikuwa na uwazi na ilifuata utaratibu wa Mikataba ya Kimataifa ya Concession Contract yaani Mkataba wa kujenga na Ku endesha ( Build and Operate) lakini baada ya Kampuni kupitia Taratibu zote za Sheria ya Nchini mathalan Taratibu zinazotakiwa kwa “ Foreign Investor”.

Kwa Tanzania ni kinyume kabisa ambapo Bandari zote zinapangwa kukabidhiwa kwa DP World, kwanza IGA, na baadaye kupitia HGA ambayo kwa utaratibu wake wala haihitaji kupitia Bungeni. Watanzania lazima tuamke. Tumepigwa tayari kama walivyozoea kutupiga kwenye Mikataba Richmond/ Dowans, IPTl/ Escrow Account, Ubungo Symbion na mingine Mingi.

Nchi kama Canada, kabla ya kuingia kwenye Mikataba ya Biashara licha ya Sheria kali, kwa mfano “ under the Federal Bank Act ..”no Person may own and Control more than 10% of shares of a “ Bank Listed” in a shedule..” Hili linalenga kulinda usalama wa Taifa lao. Aidha, Sheria ya Marekani, Canada, (Taz. Doing Business in Canada,Regulation Update 21st October, 2021), Uingereza Antwerp( Rejea Prospectus dated 1st September,2019) ambazo zina Utaratibu ulio wazi, yaani “ Base Prospectus to Investors” nilizozikagua zinahitaji utaratibu “ Very Rigorous” wa kufanya “Due Dilligence”.

Kwa Tanzania, DP World sijui kama ilifanyiwa Due diligence na vilitumika vigezo gani! Angalau utatibu uliotumika Kuipata Kampuni ya DP World unaofahamika ni kuwa walikutana kwenye Dubai Expo, 2022. Ni jambo la hatari sana. Wenzetu wanafanya Due diligence. Hi ni tofauti kabisa na Serikali ya Tanzania ambapo sasa baada ya IGA kusainiwa na Azimio la Bunge kupitishwa ndio wanahaha kuwaendea Wadau mbalimbali kutafuta kuungwa mkono.

Ikumbukwe kuwa, kwa wenzetu, mambo yote kama risk analysis, Financial Guarantees, Cash flows, discount rates, estimates of usefulness na value ya property wanayomiliki , plant and equipment, concession Rights ni mambo yote yanayojadiliwa na Wadau wote. Kwa Tanzania hata Wabunge, wenye jukumu la kuamua kwa niaba ya Taifa na Wananchi, ni “taboo” kujadili mambo hayo.

Kwa nchi za Wenzetu, kwa mfano Marekani, IGA siyo tu inasainiwa baina ya Federal Government na nchi za kigeni, bali pia baina ya States ( State moja na nyingine) , lakini pia baina yaCounty na County. Kwa mfano County ya Boulder ambayo imeweka saini mkataba IGA na Routt County. Sisi kwetu IGA ni kitu cha siri kubwa sana.

Kwenye nchi za demokrasi, pamoja na Azimio la kuridhia IGa Bunge lingelipewa Maelezo ya kina ya Lengo Kuu, Ramani ya kazi zote zitakazofanyika na Malengo yote ya IGa ( Tz. Boulder County IGA), ukubwa wa ardhi itakayohusika, gharama za fidia ya Ardhi na mali zote katika eneo la Mradi, kwa Tanzania hayo ni Siri, mpaka pale ardhi ya Wananchi itakapochukuliwa, na bila uhakika wa Fidia kama ilivyotokea Maeneo ya Kimara ambapo wananchi wameondolewa katika Maeneo yao bila utaratibu unaoonekana. Watanzania lazima tufike Mahali tukatae uonezi huu kutoka kwa Serikali ambayo kikatiba Ina jukumu la kutulinda sisi na mali zetu.

Ndugu Waandishi, ni dhahiri kwa maelezo haya huu ni Mkataba mbovu labda haijawahi kutokea katika Historia ya Taifa letu. Watanzania tumekuwa na ujasiri kujisifu kuwa na nchi nzuri, nchi ya amani na utulivu na nchi yenye rasilimali nyingi kiasi cha kufikiri ile “Eden” inayotajwa na Vitabu Vitakatifu Labda ndiyo Tanzania. Kwa bahati mbaya sana pamoja na mazuri yote hayo nchi yetu ni moja ya nchi zenye watu maskini sana, Nchi yenye huduma mbovu za kijamii yaani watoto wetu kwenye maeneo mbalimbali wanakaa chini bila viti na madawati, wamama zetu wanajifungulia kwenye mazingira magumu sana wakati Serikali ikijinasibu kujenga Hospitali kila mahali.

Ujenzi wenyewe ni kwa fedha za Mkopo. Lakini inatisha zaidi pale mama anapohitaji operation ya Uzazi wa kuokoa maisha yake na ya kichanga tumboni mwake anaambiwa alipie Tshs 200,000. Iwapo Tumboni ana Mapacha basi atalipia Tshs 200,000 kwa idadi ya mapacha. Hi ini dhambi hata kwa Mungu, viongozi wanahitaji kujitafakari, kwenye mambo mengine “ Hujionyesha malaika” lakini kuokoa maisha ya Binadamu, raia zao kamwe husikii wakitoa hata neno.

Binadamu wanakufa kwenye mazingira ya ajabu, utadhani nchi haina viongozi, alimradi Uonevu katika Ardhi, Hifadhi za Taifa, kupanda gharama za maisha kiholela naUfisadi na uwizi wa Mali za umma katika ngazi zote yote hayo yamegeuka Majanga ya Taifa. Lakini Nchi “bado inaitwa Tajiri” yenye kila aina ya rasilimali iliyoko chini ya Jua. Sijui tumelaaniwa au nini! Sijui tumekosa nini! Ninaogopa Wajukuu zetu watakuja kutupima akili zetu kuona kama kweli tu binadamu tuliokamilika.

Ndugu Waandishi, Wanasheria wa Serikali hawakuona kabisa. Madhara ya kif. Cha 10 cha IGA kwamba hata “ Serikali ya chama kingine kita kaposhika dola hakiwezi kubadilisha mkataba huu” . Hi ini kutengeneza mgogoro, kwa sababu hakuna chama kinategemewa kutawala milele. Hadi sasa uzoefu unaonyesha vyama bilivyodumu sana vimetawala kwa miaka isiyozidi 70. Sidhani kama hali itakuwa tofauti kwa Tanzania. Inawezekana hali hii ya Watanzania wengi kuunganisha nguvu ni dalili kuendea historia hiyo ya Vyama Tawala

Kifungu cha 21 kinakwenda kinyume na Sheria ya “National Wealth….. na hivyo haikubaliki, kifungu cha 23 kinaleta utata mkubwa kwa kuwa muda wa Mkataba haujatajwa bali unategemea “ Permanent Cessation of all project activities expiration of all HGAs and all of the project agreements. Hiki kifungi ni cha hatari na hakikubali.

Natambua tatizo ni kuwa Bandari etce zilivyowekwa zinaweza kuchukua hata miaka 1000. Mkataba wa aina hii bila kupepesa macho ni mkataba mbovu na hivyo haukubaliki. Kifungu cha23(4) ambacho kinatumia “ State Parties SHALL not be entittled… in any circumstances including in the event of material breach, change of curcumstances…” nacho hakikubaliki kabisa.

Ndugu Wanahabari, baada ya Maelezo hayo sasa niseme yafuatayo kwa kifupi sana:
1) Kwa lugha Rahisi sana, Taarifa hii haina lengo la kupinga Uwekezaji au maboresho au mambo mapya yanoyoenda kufanyika kuboresha Katika Bandari yetu. Hoja ya ya msingi ni kukosekana kwa uwazi katika namna ya kushughulikia Rasilimali Muhimu kama Bandari. Tunao jali hatuwezinkukaa kimya tukiona mambo yana haribika, Hoja zetu zinasukumwa na uzoefu wa miaka mingi ambapo takriban katika kila mradi kumekuwa na “Upigaji mkubwa”, wakati Taifa letu na Wananchi wake wakiendelea kuogelea katika Lindi la Umaskini.

Kila Mtanzania mwenye akili, mwenye Busara na mwenye mapenzi ya dhati kwa Watanzania wenzake hawezi kukaa kimya wakati kundi dogo sana lililoko Serikalini likineemeka. Nimetoa mifano yote kwa yule mwenye nia ya kudadavua na kupima ninayoyaeleza hapa.

2) Hoja hapa ni hatua hiyo, ambayo katika sura yake halisi, kwa mtu mwenye upeo wa kuona mbali, Rasilimali hii muhimu ( Bandari za nchi nzima) zinaenda kubinafsishwa kwa Kampuni binafsi, ambayo katika sura yake halisi Ni kitu kimoja na ni sehemu ya Uongozi wa Taifa la nje. Kwa mtu mwenye busara japo kidogo huwezi kubinafsisha, kwa utaratibu unaoelezwa na IGA, yaani Bandari zote za Tanzania Bara, zilizoko na zitakazojengwa, njia za Reli zinazohusiana na huduma za Bandari na Uwanja wa Ndege.

Kwa Taifa lolote hizi Taasisi nyeti na muhimu kwa uhai wenyewe wa Taifa. Unakabidhi hayo maneno nyeti, hivi siku mkikorofishana; kwani duniani historia inaonyesha hakuna urafiki wa kudumu, si tumeuweka Usalama wa Taifa letu “Rehani”. Ni kwani mambo makubwa hivyo yanafichwa, Wananchi katika Tafsiri halisi Katiba aibara ya 8(c ). Mbona kwenye Serikali ya awamu ya kwanza miaka. Ya 1960 hadi miaka ya 1980 Watanzania Walishirikishwa mpaka vijijini katika utengenezaji wa Sera mbalimbali. Watanzania wa leo ni tofauti. Mbona katika Usiri ufisadi ndio umekithiri zaidi

3) Jambo ambalo limeleta taharuki, ni hali ya Bandari za Tanganyika tu ndio zinahusishws na Bandari za Zanzibar hazipo kwenye mpango huo. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano hapigiwi kura na Upande wa Zanzibar. Mimi ninaelewa tatiza ni kuwa japo Katiba yetu inatambua kuwa Tanzania ni moja, na kuna Mambo ya Muungano na Mambo yasiyo ya Mungano. Lakini katika Swala la bandari na Mamlaka za uendeshaji wa Bandari Serikali imejikanyaga, kwa kuruhusu Sheria mbili zinazoongoza Mamlaka za Bandari wakati Katiba hajarekebishwa. Wananchi wakilalamika msistuke kwa sababu baadhi ya mambo mmeyasababisha wenyewe Serikali, au kwa uzembe, au kwa kukosa umakini, au kwa wahusika kutotekeleza majukumu yao. Mnayo listi ya Mambo ya Mungano lakini hamuiheshimu. Kwanini basi isiondolewe ndani ya Katiba ya JMT?

Hivyo Basi,

1) Natoa wito kwa Watanzania wote, popote waliopo, bila kujali hali zetu, Wasomi, wafanyikazi, Watoto wa Shule( Viongozi wetu wa siku zijao) wakulima, wafugaji, wavuvi, Vyama vya Siasa, Vyama vya Hiari na NGO zote, Madhehebu ya Dini, sote kwa pamoja tusikubali kupokea upotoshwaji wa aina yeyote katika mambo yanayotuhusu sisi wenyewe, na vizazi vyetu vijavyo. Tusimame kidete, tupige kelele kulinda mali yetu. Rasilimali hizi tumepewa na Mwenyezi Mungu, ni jukumu letu sote kuzilinda sisi wenyewe iwapo tuliowakabidhi madaraka wameshindwa, Taarifa za kila mwaka za CAG ni Kielelezo cha wazi, kuwa Matrilioni yanayopotea, au kuibiwa, au hayajulikani yalipo. yangelitiririka kwa mfumo unaotakiwa leo kila Mtanzania angekuwa analala kwenye nyumba bora, yenye Maji tiririka ndani. Watoto wetu wangelikuwa wanasoma shule bora na siyo bora shule na sote tungelikuwa tunapata matibabu bora

2) Kwa Kutambua hayo Natoa Mwito kwa viongozi, kwa Mheshimiwa Rais, dosari za wazi katika Mkataba huu ziondolewe, Ili Mkataba huu uweze kuendelea katika hatua za awali na iwapo Kampuni husika tutaridhika nayo Mkataba uongezwe kwa jinsi tutakavyowapima na kwa kila hatua kuzingatia Maslahi ya Usalama wa Taifa letu.
3) Iwapo baada ya Siku 30 Serikali haitaonyesha nia njema, na kuchukua hatua madhubuti ya kurekebisha hizi dosari, Wananchi kwa mujibu ya Katiba ni uhuru wenu kuchukua hatua mtakazoona zinafaa kwa Mujibu wa Katiba yetu. Natambua Maandamano ni haki ya Kikatiba alimradi tunarejesha mamlaka yaliyopokwa na Serikali kutoka mikononi mwa Wenye Nchi wenyewe!

Nawashukuruni kwa kunisikiliza

Balozi Dr Willibrod Peter Slaa

Zaidi soma Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Bunge letu tulilolipa dhamana ya kutuwakilisha lenyewe Lina kazi ya kujibu na kuitetea serikali na kuwakemea wananchi Kama mh. nape
Jamani kina Siku swala hili litaivia serikali nguo na watageukana, na adhabu itakuwa kung'atuka kwa baadhi ya Mawaziri Basi
Au watakuja kuanza kubadili baadhi ya vifungu kwa kusema wao ni wasikivu.
Qn bongo ni siasa na siasa ni bongo discuss.
Tunza maneno yangu
 
Book on Dr Slaa's history in offing | The Citizen's history in offing | The Citizen

Kazi ni kutetea gavoo na kuwakemea wanaotetea maslahi ya Taifa!!
 
Pamoja na yote Dr yupo sahihi kbs ✔️!! Ingawa uzi huu ni mwiba kwa wanaccm wote wakiongozwa na Johnthebaptist, GUSSIE, Lord denning, Faizafoxy and co.
 
Katika hili jambo,CCM imejiweka pabaya sana ktika chaguzi kuu zijazo Sijui nini kitafanyika

kurudisha hao wabunge waliopo BUNGENI ukisikia ukiinama nchale ukiinuka nchale ni uchaguzi ujao

haya madudu yanayoendelea sijui kama wamewaza namna ya kujisafisha kwa wananchi wakija kuomba Kura.

Moja kati ya dosari kubwa iliyotia Muhuri utendaji mbovu/mbaya/wa hovyo wa serikali ya awamu ya 6,Heri wenye

akili kama kina slaa waliogoma kuwa Kenge kwenye msafara wa Mamba,waliobaki wote wanatetea matumbo yao TU.
 
Bunge letu tulilolipa dhamana ya kutuwakilisha lenyewe Lina kazi ya kujibu na kuitetea serikali na kuwakemea wananchi Kama mh. nape
Jamani kina Siku swala hili litaivia serikali nguo na watageukana, na adhabu itakuwa kung'atuka kwa baadhi ya Mawaziri Basi
Au watakuja kuanza kubadili baadhi ya vifungu kwa kusema wao ni wasikivu.
Qn bongo ni siasa na siasa ni bongo discuss.
Tunza maneno yangu
Hakuna namna ! Labda tuseme kama wahusika wana nia mbaya Mungu anawaona 🙏🙏
 
Katika hili jambo,CCM imejiweka pabaya sana ktika chaguzi kuu zijazo Sijui nini kitafanyika

kurudisha hao wabunge waliopo BUNGENI ukisikia ukiinama nchale ukiinuka nchale ni uchaguzi ujao

haya madudu yanayoendelea sijui kama wamewaza namna ya kujisafisha kwa wananchi wakija kuomba Kura.

Moja kati ya dosari kubwa iliyotia Muhuri utendaji mbovu/mbaya/wa hovyo wa serikali ya awamu ya 6,Heri wenye

akili kama kina slaa waliogoma kuwa Kenge kwenye msafara wa Mamba,waliobaki wote wanatetea matumbo yao TU.
Masikini bado unaamini ktk uchaguzi.
Eti CCM itegee kura zetu!!
 
Jamii forum nipende kuwashukuru kwa kuweka taarifa kamili kwani ninachokisoma kwenye magazeti ni tofauti kabisa. Kwa ninavyoona wandishi wa Habari wameamua kuupotosha umma juu ya kilichoongelewa na Dr.
 
Hakuna namna ! Labda tuseme kama wahusika wana nia mbaya Mungu anawaona
Aiseee! Bado huelewi, baada ya maelezo yote haya aliyotoa Dr Slaaa?

Watakuwaje na "Nia Mbaya", wakati hata hawakutaka waTanzania wajue kilichomo kwenye mkataba?
Wewe huoni "NIA NZURI" kabisa ya hawa wazalendo wa nchi yetu?

Watu wa aina yako sijui tuwafanye nini ndipo muweze kuelewa?

Nakupa pole yako na kukuheshimu, kwa sababu najua wakati mwingine huwa unajitambua sana na kutambua maslahi ya taifa lako.
Nasema hivyo, kwa sababu nilishakutana nawe mara kadhaa humu JF na kukubali hoja zako.
 
Back
Top Bottom