Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 516
- 1,348
Habari ndugu zangu wote,
Nipo hapa kuwapa taarifa ya maendeleo ya matibabu ya Edgar Edson Mwakabela (@Sativa255) ambaye anapata matibabu The Aga Khan Hospital, Dar es Salaam.
Kutokana na vipimo vikubwa vya madaktari wabobezi wa The Aga Khan Hospital, Dar es Salaam, walitueleza ni muhimu akafanyiwa upasuaji mkubwa katika taya.
Ni upande uliathirika baada ya kupigwa risasi, alfajiri ya siku ya Alhamisi, Juni 27, 2024 katika moja ya mapori yenye wanyama wakali katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Leo, Jumanne, Julai 02, 2024 ni siku ambayo ndugu yetu, SATIVA atafanyiwa upasuaji (operation) katika sehemu hiyo ya taya (kushoto) ambayo iliathiriwa na risasi.
Hii inaitwa 'Mandibular fracture/fracture of the jaw'. Kuvunjika kwa mandibular, pia inajulikana kama kuvunjika kwa taya, ni kupasuka kwa mfupa wa mandibular.
Hii inaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufungua kinywa kikamilifu. Kupanua mdomo. Na jambo hilo limempata ndugu yetu SATIVA. Hapanui mdomo.
Upasuaji huo una gharama zake kubwa kutokana na kwamba ni upasuaji mkubwa ambao unahitaji utaalam wa hali ya juu sana. Madaktari wamesema wataufanya tu.
Gharama ya matibabu hadi sasa jumla ni takribani Tsh. 33,000,000. Ni upasuaji na huduma za kulazwa tangu amepokelewa kutoka Muhimbili National Hospital (MNH)
Katika fedha hizo, zimelipwa Tsh. 14,000,000/-. Michango kutoka kwa wadau na narafiki ni kiasi cha Tsh. 10,000,000/-. THRDC wamechangia Tsh. 4,000,000/- hadi sasa.
Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) wao wametoa ahadi kwamba watachangia kiasi cha Tsh. 19,000,000 iliyobaki katika gharama za upasuaji.
Ni nje ya gharama nyingine nyingi zikiwepo kuanzia Hospitali ya halmashauri ya Mpimbwe baadae Hospitali ya Rufaa Mkoa Katavi na gharama za usafiri wa mgonjwa.
Gharama hizo tajwa juu kwa jumla yake ni takribani Tsh. 5,000,000. Hizi ni fedha kutoka kwa wadau mbalimbali nje ya michango yetu ya pamoja wanajumuiya ya 𝕏.
Makubaliano yetu;, fedha za michango ya wanajumuiya ya 𝕏 ambayo ni Tsh. 13,765,000 itahusika katika kumuuguza mgonjwa akitoka The Aga Khan Hospital, nyumbani.
Hivyo, tunaweza kuendelea kuchanga, michango yetu na itamsaidia sana SATIVA kujigusa katika matibabu yake baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali. Tusichoke.
Naendelea kutoa shukrani zangu za dhati kwenu wote wana-jumuiya ya 𝕏 (wakiongozwa na Miriam Mkanaka) na THRDC na wengine wengi tu kwa kuguswa na jambo hili.
Hakika mmegusa maisha ya SATIVA. Nimezungumza na ndugu yetu kwa kirefu sana, ikafika wakati akaanza kulia kwa machozi ya shukrani na furaha kubwa.
Wazazi wa Edgar Edson Mwakabela hawana cha kuwalipa, isipokuwa wanatuma shukrani zao za dhati na kuwaombea wanajumuiya wote. Hakika, wanawashukuru sana.
Ahsante. Nitaendelea kuwapa taarifa. 🙏
Martin Maranja Masese, MMM.