Ni mwezi sasa umepita toka mwaka watatu batch 1 wafungue chuo, katika chuo kikuu cha mtakatifu Joseph. Lakini hadi sasa hivi bado hawajapokea mkopo yao kama meals and accomodation. Vijana wanaishi kwa shida sana.
Imefika hadi hatua wanafukuzwa na wenye nyumba. Mara ya mwisho wanafunzi hawa kupokea boom ni April mwaka jana. Maisha yamekuwa magumu sana kwao, tunaomba serikari ingilie kati.
Wakati vyuo vingine wanamaliza mwezi July, kwa st Joseph university ni tofauti mwaka watatu watamaliza December tarehe 2, hii inamanisha nini? Kumbuka hawa vijana wanasomea taaluma ya uwalimu wa science, hii itapelekea wao kukosa ajira ya serikari.
Tunaomba serikari ingilie kati. Na kama kuna mtu yupo wizara ya elimu na TCU hafikishe taarifa hizi. Mana vijana wetu wanaishi maisha magumu sana na hawana hata matumaini ya kesho.