KERO Taa za kwenye Kituo cha Mwendokasi-Gerezani hazifanyi kazi, abiria tunatumia tochi za simu kwa ajili ya usalama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
280
478
Licha ya kero mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na Wananchi wenzangu kwa nyakati tofauti kuhusu Mwendokasi, lakini kuna kero ambayo imejitokeza kwa zaidi ya wiki sasa na haijapatiwa ufumbuzi wa haraka.
IMG-20250327-WA0023.jpg

Katika kituo hicho kumekuwepo na malalamiko ya Wananchi kuibiwa simu zao na kuporwa mikoba kwenye kituo nyakati za usiku kutokana na taa za kwenye kituo hicho kutofanya kazi, kwa sasa Wananchi tunaoingia kwenye kituo hicho usiku tunalazimika kuwasha tochi za simu ili kujilinda waporaji.

Kwakweli hili jambo limenigusa sana siwezi kulinyamazia maana ni uzembe wa hali ya juu, najiuliza kweli mamlaka zinazosimamia miundombinu ya vituo hawana taarifa juu ya changamoto hiyo. Mimi nadhani wanatakiwa kuwajibika kwa uzembe.

Ni muhimu tukatambua kwamba kero hii inagusa usalama wa abiria na mali zao, sio jambo ambalo nilitegemea kuona mamlaka husika zilifumbia macho kwa kuchelewa kulitafutia ufumbuzi.
IMG-20250327-WA0014_1.jpg
Nitoe wito kwa mamlaka za juu hasa TAMISEMI kufuatilia suala hili ili watakaokuwa wamebainika walishindwa kuwajibika ipasavyo kuwajibika ipasavyo wachuikuliwe hatua za kisheria.
IMG-20250327-WA0016_1.jpg
 
Back
Top Bottom