Swali Kwa Wizara ya Afya/Ustawi wa Jamii: Kwa Nini Msiratibu Zoezi la Kutambua Watu Wote wenye Changamoto Kubwa za Afya Ili Jamii Isaidie Matibabu?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
54,347
64,376
Nimekuwa naona kampeni mbalimbali zinazofanywa na taasisi na mashirika binafsi wakitumia mbio za marathon ,mabonanza nk kwa lengo la kuchangisha pesa kusaidia watu wenye shida kubwa hasa Watoto kwenye maeneo ya moyo nk.

Kitu kinachonishangaza inakuaje Wizara ya Afya,na Ile ya Ustawi wa Jamii,Jinsia na wenye ulemavu wasiungane na hao kuandaa kampeni ya Nchi nzima Ili kutambua watu hao na pia kujua gharama zinazotakiwa kuwatibh Ili Serikali na jamii ichangie?

Magonjwa kama hayo Kwa mtu wa kawaida sio rahisi kuyamudu peke yake.Just imagine Mbunge na msanii mkubwa na Maarufu alilazimika.kuomba Msaada wa jamii na Kwa jina lake akasaidiwa sio tuu na jamii Bali na Rais ,vipi Kwa watu wasio Maarufu kama Hawa ambao wanajitokeza kwenye ziara za Viongozi?

Kiukweli ni vyema Wizara husika mkachukua ushauri huu ,kama sekta binafsi inaweza nyie mnashindwa nini?

Naomba kuwasilisha 👇👇

View: https://twitter.com/MwanaHabariNews/status/1813916763626844268?t=1m_cqLhXCea1wmNFoOdmZA&s=19
 
Back
Top Bottom